top of page

Majadiliano na Wataalamu

Public·804 members

Mate meupe kama maziwa asubuhi??

Ni nini husababisha kutokwa na mate meupe kama maziwa??

568 Views

Mate kuwa meupe kama maziwa fresh, au maziwa mgando wakati wa asubuhi huweza kusababishwa na sababu mbalimbali. Kisababishi kikubwa ni kuzaliana kwa fangasi kupiti kiwango cha kawaida katika kinywa. Dalili zingine zinaweza kuambatana na tatizo hili la fangasi wa kinywa ambazo zimeorodheshwa katika makala ndani ya tovuti hii. Soma zaidi kuhusu fangasi wa kinywa/ulimi kwa kubonyeza hapa.


Visababishi vingine ni


  • Tatizo la kukauka kwa kinywa (kinywa kikavu)

  • Matumizi ya dawa za kukausha mate

  • Matumizi ya dawa za antibiotics zinazoua bakteria rafiki wa kinywa na

  • Sababu zisizofahamika.


Wasiliana na daktari wako kwa uchunguzi zaidi na tiba endapo una tatizo hili

Kuhusu kundi

Uliza swali pamoja na kusoma majibu ya maswali yaliyoulizwa,...

bottom of page