top of page

Majadiliano na Wataalamu

Public·804 members

Tumbo la ujauzito huanza kuonekana lini?

Kwa kawaida tumbo la ujauzito huanza kuonekana katika kipindi cha pili cha ujauzito kuanzia wiki ya 16 hadi 27 na kuendelea. Baadhi ya wanawake hata hivyo huchelewa kuonyesha tumbo mpaka kufikia kipindi cha tatu cha ujauzito, haswa kwa wanawake wanene kupindukia au wenye maji kidogo katika chupa ya uzazi.


Baadhi ya wanawake pia huweza kuonyesha tumbo la ujauzito mapema, mfano ni wanawake ambao wameshajifungua zaidi ya mara moja, wenye mimba ya mapacha au maji mengi katika chupa ya uzazi.


Wakati gani uwe na hofu?

Unahitaji kuwa na hofu na kuongea na daktari endapo tumbo la ujauzito halijaonekana mpaka unapofikia kipindi cha tatu cha ujauzito. Kunaweza kuwa na sababu mbalimbali kutoka kwa mama au mtoto zinazoweza kuchangia kutoonekana au kuonekana mapema kwa tumbo. Kuonana na daktari kutaondoa hofu na kukufahamisha kama mujauzito unaendelea vema au la.


Wapi unaweza kusoma zaidi

Pata maelezo zaidi kwa kuwasiliana na daktari wako, unaweza kutembelea makala zifuatazo kujielimisha kuhusu tumbo kubwa kupita kiasi katika ujauzito( tumbo kubwa la ujauzito) kutokana na maji mengi katika chupa ya uzazi na tumbo dogo kupita kiasi katika ujauzito( tumbo dogo la mimba) kutokana na maji kidogo kwenye chupa ya kizazi.


Makala zingine zinazohusu ujauzito

Rejea za mada hii:


  1. WEBMD. https://www.webmd.com/baby/when-do-pregnant-women-start-showing. Imechukuliwa 02.10.2024

  2. Maji kidogo kwenye chupa ya uzazi. https://www.ulyclinic.com/magonjwa-na-saratani/maji-kidogo-kwenye-chupa-ya-uzazi. Imechukuliwa 02.10.2024

  3. Maji mengi kwenye chupa ya uzazi. https://www.ulyclinic.com/maji-mengi-kwenye-chupa-ya-uzazi. Imechukuliwa 02.10.2024

164 Views

Kuhusu kundi

Uliza swali pamoja na kusoma majibu ya maswali yaliyoulizwa,...

bottom of page