top of page

Majadiliano na Wataalamu

Public·804 members

Inachukua muda gani kupona kaswende?

Inachukua muda gani kupona kaswende baad aya kuanza kutumia dawa?

163 Views

Inaweza kuchukua muda wa wiki mbili hadi siku 28 kupotea kwa dalili za kaswende, hii inategemea na kaswende ina muda gani;


  • Kaswende iliyodumu chini ya miaka miwili, hutibiwa na dawa za kuchoma kwenye kalio jamii ya penicillin kwa muda wa siku 10 hadi 14 na baada ya muda huu utasemekana kuwa umepona kwani dalili zitapotea

  • Kaswende iliyodumu kwa muda zaidi ya miaka 2 hutibiwa kwa dawa za kuchoma kwenye kalio kila wiki kwa muda wa wiki tatu, au kunywa vidonge kwa muda wa siku 28. Baada ya muda huu utasemekana kuwa umepona kwani dalili zitapotea

  • Kaswende ambayo ni ya hatari na imeathiri ubongo hutibiwa kwa kuchomwa sindano kila siku kwa muda wa wiki mbili au kunywa dawa za kumeza kwa muda wa siku 28. Baada ya muda huu utasemekana kuwa umepona kwani dalili zitapotea


Soma zaidi kuhusu kaswende kwa kubofya hapa

Kuhusu kundi

Uliza swali pamoja na kusoma majibu ya maswali yaliyoulizwa,...

bottom of page