top of page

Majadiliano na Wataalamu

Public·804 members

Dalili za mimba baada ya kutoa mimba

Baada ya kutoa mimba, dalili za mimba huendelea kupungua na kuisha kabisa, mabadiliko haya ya dalili huendana na kiwango cha homoni ya ujauzito mwilini yaani bHCG. Homoni bHCG kwa kawaida hupungua kwenye damu kwa jinsi siku zinavyoenda baada ya kutoa mimba. Dalili zote za mimba zinazoonekana hutokana na uwepo wake na endapo homoni hii bado inaongezeka kwenye damu humaanisha mimba bado inaendelea.


Dalili za ujauzito baada ya kutoa mimba

 

Je, inachukua muda gani kwa dalili za mimba kuisha baada ya kutoa mimba?

Kwa kawaida, huchukua siku 2 hadi 14 kwa dalili za mimba kupotea na kuisha kabisa baada ya kutoa mimba, hata hivyo baadhi ya wanwake wanaweza kuendelea kuona dalili ambazo si kali hadi wiki 4 baada ya kutoa mimba kama kuna masalia ya tishu za mimba kwenye kizazi au kama alikuwa na ujauzito wa zabibu. Dalili za chuchu kuvimba na kuuma mara nyingi huchukua muda mrefu kuisha kati ya dalili zote za ujauzito.


Dalili hii mara nyingi hupotea mwishoni
Chuchu kuvimba

 

Je, Dalili za mimba baada ya kutoa mimba ni zipi?

Dalili za mimba baada ya kutoa mimba zinaweza kuwa katika makundi mawili, yaani dalili za mimba inayoendelea baad ya kutoa mimba, na dalili za mimba iliyoingia baada ya kutoa mimba. Maelezo ya dalili hizo ni kama ifuatavyo:

 

Dalili za mimba inayoendelea baada ya kutoa mimba

Kama mimba imeshindwa kutoka, dalili za mimba zilizokuwepo awali zitaendelea kuonekana na kuongezeka kwa jinsi homoni bHCG inavyoongezeka kwenye damu. Dalili hizo huwa pamoja na:

  • Kichefuchefu bila kutapika

  • Mabadiliko kwenye chuchu

  • Kukojoa mara kwa mara

  • Maumivu ya kichwa

  • Ongezeko la joto la mwili

  • Hisia za gesi tumboni

  • Maumivu ya wastani ya nyonga

  • Uchovu mkali

  • Kubadilika hali ya hali ya moyo (Hisia)

  • Kupendelea chakula aina fulani tu

  • Ongezeko la hisia kwenye harufu

  • Kuhisi ladha ya umetali

 

Dalili za mimba mpya baada ya kutoa mimba

Baada ya kutoa mimba, unaweza kushika ujauzito mwingine ndani ya wiki 1 hadi 4 tangu mimba imetoka ikitegemea idadi ya siku katika mzunguko wako hedhi. Mimba ikitungishwa wakati huu hupelekea kuonekana kwa dalili zifuatazo;

  • Homa wakati wa asubuhi

  • Kichechefu na kutapika

  • Kubadilika rangi ya chuchu na kuwa na weusi uliokolea

  • Kuumwa kwa matiti

  • Hisia za uchovu

  • Mwili kulegea

  • Kukojoa mara kwa mara

  • Kubadilika kwa hisia ya moyo(kuwa na huzuni au furaha)

  • Kuvuruga kwa tumbo

  • Mafua

  • Maumivu ya kichwa

  • Kuchagua vyakula

  • Kukosa hamu ya kula

  • Hisia ya kizunguzungu

  • Kuzimia

Dalili zingine zinazoonekana kwa mimba ya zaidi ya mwezi mmoja

Dalili zingine amabazo huonekana baada ya mwezi mmoja kupita ni kama zifuatavyo

Kutoingia mwezini (kutoona damu ya hedhi)

  • Tumbo Kuongezeka

  • Hisia za mtoto kucheza tumboni katika wiki ya 16 na kuendele

  • Kupata haja ngumu

  • Kubadilika kwa ngozi

Wapi unaweza kupata maelezo Zaidi kuhudu dalili za mimba baada ya kutoa mimba?

Unaweza kupata maelezo Zaidi katika makala ya dalili za mimba katika miezi kwa kubofya linki za Makala zifuatazo.

 

Mambo mengine unayopaswa kufahamu baada ya kutoa mimba

Kwa kuwa baada ya kutoa mimba unaweza kupata mimba nyingine mara moja, utapaswa kutumia kinga ili kuzuia mimba. linki ifuatayo ina video zinazoainisha siku za hatari kulingana na mzunguko wako wa hedhi. Bofya kiungo cha makala husika hapa chini ili kufahamu ni lini unaweza kushika ujauzito hivyo ujikinge.



Rejea za mada hii

  1. Abortion Clinics Amsterdam & Haarlem. After the day treatment or abortion pill. https://www.bloemenhove.nl/en/aftercare/after-the-treatment/#. Imechukuliwa 16.11.2024

  2. van der Lugt B, et al. The disappearance of human chorionic gonadotropin from plasma and urine following induced abortion. Disappearance of HCG after induced abortion. Acta Obstet Gynecol Scand. 1985;64(7):547-52. doi: 10.3109/00016348509156360. PMID: 2417443.

  3. Parents. What to Expect After an Abortion. https://www.parents.com/pregnancy/complications/your-body-after-abortion/#. Imechukuliwa 16.11.2024

  4. ULY CLINIC. Dalili za mimba ya mwezi mmoja. https://www.ulyclinic.com/umri-wa-mimba-kwa-miezi/mimba-ya-mwezi-mmoja. Imechukuliwa 16.11.2024

870 Views

Kuhusu kundi

Uliza swali pamoja na kusoma majibu ya maswali yaliyoulizwa,...

bottom of page