top of page

Majadiliano na Wataalamu

Public·804 members

Kinyesi chenye kamasi

Kupata kinyesi chenye kamasi isikufanye uogope sana kwa kuwa mara nyingi ni hali ya kawaida. Kinyesi kwa kawaida kina kiwango kidogo cha kamasi ambacho husaidia kiweze kupita kirahisi kwenye utumbo mpana na kutoka nje.


Wakati gani wa kuhofia unapokuwa na kinyeshi chenye makamasi?


Unapaswa kuwa na wasiwasi endapo kinyesi chenye kamasi kimekuwa na sifa zifuatazo;


  • Kamasi kuwa nyingi zaidi ya kawaida

  • Kamasi kuwa na michirizi au matone ya damu

  • Kimeambatana na mabadiliko ya tabia ya tumbo kama maumivu ya tumbo n.k


Sababu gani zinaweza kusababisha kamasi kwenye kinyesi?


Kamasi kwenye kinyesi huweza sababishwa na;


  • Maambukizi mfumo wa umeng’enyaji chakula

  • Ugonjwa wa crohns

  • Ugonjwa wa asaletive kolaitiz

  • Saratani ya utumbo mpana


Kinyesi chenye kamasi kwa watoto


Visababishi vya kinyesi chenye kamasi kwa watoto vinaweza kuwa;


  • Sindromu ya iritabo baweli

  • Intusasepusheni

  • Asaletivu kolaitiz

  • Sistiki fibrosisi

  • Maambukizi tumboni ( amiba n.k)

  • Vidole kwenye utumbo

  • Mzio na chakula

  • Kutostahimili chakula

  • Kuharisha sana

  • Mabadiliko ya kunyonya maziwa


Rejea za mada hii;


Soma zaidi kwenye Makala ya ‘kinyesi chenye kamasi kwa mtoto’ na ‘kinyesi chenye kamasi kwa mtu mzima’ kwa uelewa zaidi.


  1. LaRocque R, et al. Approach to the adult with acute diarrhea in resource-rich settings. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 28.06.2021

  2. Stone CK, et al., eds. Pediatric emergencies. In: Current Diagnosis & Treatment: Emergency Medicine. 8th ed. New York, N.Y.: McGraw-Hill Education; 2017. http://accessmedicine.mhmedical.com. Imechukuliwa 28.06.2021

  3. Intussusception. https://pedclerk.bsd.uchicago.edu/page/intussusception. Imechukuliwa 28.06.2021

  4. P Dutta, et al. Mucoid presentation of acute enterocolitis in children: a hospital-based case-control study. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/10503679/. Imechukuliwa 28.06.2021

  5. Zixiang Li,et al. Prospective Study on the Excretion of Mucous Stools and its Association with Age, Gender, and Feces Output in Captive Giant Pandas. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC6562534/. Imechukuliwa 28.06.2021

14040 Views

Führerscheine Kosten

Suchen Sie nicht weiter als unter https://legaldocumentseu.com/, Ihre Go-to-Quelle für Premium-Fälschungen, Führerscheine Kosten und IDs.

https://legaldocumentseu.com/

Kuhusu kundi

Uliza swali pamoja na kusoma majibu ya maswali yaliyoulizwa,...

bottom of page