top of page

Majadiliano na Wataalamu

Public·804 members

Siku za mzunguko wa hedhi

  • Mwanamke anawezaje kufahamu idadi ya siku za mzunguko wake wa hedhi?

  • Mwanamke anawezaje kufahamu kuwa ana mzunguko wa hedhi wa siku 21, 28 , 31 au 32?

  • Idadi ya siku za mzunguko wa hedhi hutambuliwaje?

259 Views

Njia za kufahamu idadi ya siku za mzunguko wa hedhi


Mwanamke anaweza kutambua idadi ya siku za mzunguko wa hedhi kuwa ni kwa kutumia kalenda au vikokoteo mbalimbali.


Matumizi ya kalenda



Namna ya Kuhesabu idadi ya siku za mzunguko wa hedhi

Ili kufahamu dadi ya siku za mzunguko wa hedhi moja na nyingine, unapaswa kuwa na kalenda yako pamoja na kalamu au penseli kisha;


Zungushia duara kwenye tarehe ambayo damu ya hedhi imeanza kutoka na tarehe hedhi itakapokata


Mwezi unaofuata zungushia mduara tena kwenye tarehe hiyo ya kuona hedhi na tarehe ya kumaliza hedhi na fanya hivi kwa angalau miezi mitatu


Baada ya kuzungushia mduara kwenye tarehe kwa kipindi cha miezi mitatu ufanyaje?


Baada ya miezi ya kuzungushia tarehe angalau kwa miezi mitatu fanya mahesabu madogo yanayofuata;


Hesababu idadi ya siku kuanzia hedhi moja kuanza hadi siku moja nyuma kabla ya hedhi ya mwezi unaofuata kuanza- idadi ya siku utakazopata ni sawa na idadi ya siku katika mzunguko wako wa hedhi wa mwezi mmoja.


Ili kupata uhakika wa idadi sahihi ya siku za mzunguko wako wa hedhi, tafuta wastani wa siku za mzunguko wa hedhi kwa kipindi cha angalau miezi mitatu yaani mfano, idadi ya siku za mzunguko wa hedhi kwa mwezi wa kwanza ulipoanza kuhesabu ni 28, idadi ya mwezi unaofuata ni 27 na idadi ya mwezi wa tatu ni 29, wastani wa mzunguko wa hedhi kwa muda wa miezi mitatu hii utakuwa sawa na;


(28+ 27+29)/3 = 84/3= 28


Hivyo mzunguko wako wa hedhi ni wa siku 28


Mahesabu ya mfano kutoka kwenye picha


Katika mwezi januari, idadi ya siku za mzunguko wa hedhi ni siku 32, mwezi februari ni siku 32 na mwezi machi ni siku 32, wastani au idadi ya siku za mzunguko wa hedhi kwa miezi mitatu ni sawa na


(32+32+32)/3 = 96/3= siku 32


Hivyo idadi ya siku za mzunguko wa hedhi ni siku 32.




Namna ya kufahamu wastani wa siku za damu ya hedhi


Ili kufahamu wastani wa idadi ya siku za damu ya hedhi, tafuta wastani wa jumla ya idadi ya siku katika miezi mitatu


Mfano mwezi wa kwanza uliingia siku 6, mwezi wa pili ni siku 4 na mwezi wa tatu ni siku 5, wastani wa siku zako za hedhi ni sawa na;


(6+5+7)/3= 18/3= 6


Hivyo wastani wa siku za damu ya hedhi ni siku 6


Je kuna faida za kufahamu idadi ya siku za mzunguko wa hedhi?


Ndio kuna faida nyingi za kufahamu mzunguko wako wa hedhi una siku ngapi hii ni pamoja na kukuwezesha kupata tarehe sahihi ya kujifungua kama ukitumia kikokoteo cha tarehe ta kujifungua na pia kujiandaa kufahamu ni lini utaingia hedhi inayofuata na lini utakuwa kwneye siku za hatari kwa kusoma kalenda yako.



Rejea za makala hii;


  1. The society of obstetric and gynecologist of Canada. Normal period. https://www.yourperiod.ca/normal-periods/menstrual-cycle-basics/. Imechukuliwa 31.07.2021

  2. Menstruation Calculator. https://healthengine.com.au/info/menstruation-calculator. Imechukuliwa 31.07.2021

  3. Menstrual Cycle. https://www.womenshealth.gov/menstrual-cycle. Imechukuliwa 31.07.2021

  4. ULY CLINIC. Mzunguko wa hedhi. https://www.ulyclinic.com/mzunguko-wa-hedhi. Imechukuliwa 31.07.2021

  5. Beverly G Reed, MD, et al. The Normal Menstrual Cycle and the Control of Ovulation. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK279054/. Imechukuliwa 31.07.2021

  6. Laurie Wideman, et al. Accuracy of Calendar-Based Methods for Assigning Menstrual Cycle Phase in Women. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3658377/. Imechukuliwa 31.07.2021



Kuhusu kundi

Uliza swali pamoja na kusoma majibu ya maswali yaliyoulizwa,...

bottom of page