top of page

Majadiliano na Wataalamu

Public·804 members

Tatizo la kuota vidonda mdomoni mara kwa mara nini kisababishi?


vidonda hivi Yaan vinaweka uduara na hutoka na kupotea,

Lakini haviponi moja kwa moja,

Vinakauka cku 3 then siku 3 vinarudi tena,

Huu mwaka ni wa pili tokea vianze,

Nimetumia antibiotik za kila aina havitoki,

Je shida inaweza kuwa nini?

145 Views

Vidonda ndani ya mdomo



Vidonda ndani ya mdomo (kinywa) hujulikana kwa majina tofauti kama kanka, au apthous ulcer. Vidonda hivi huwa ni majeraha yaliyo na kina kifupi yanayoota kwenye sehemu laini ndani ya midomo chini ya fizi au chini ya ulimi. kama inavyoonekana kwenye picha.


Vidonda hivi huwa na sifa zingine zifuatazo;


• Huweza kutokea kimoja au zaidi ya kimoja

• Haviambukizwi kama vilivyo vidonda vya homa baridi

• Havitokei nje ya midomo, wala kwenye kona za midomo kama vilivyo vidonda vingine

• Hupona ndani ya siku 7 hadi 10.


Endelea kusoma zaidi kwa kubonyeza hapa

Kuhusu kundi

Uliza swali pamoja na kusoma majibu ya maswali yaliyoulizwa,...

bottom of page