top of page

Majadiliano na Wataalamu

Public·804 members

Matapishi ya kijani

Kutapika matapishi ya kijani au njano inayoelekea kijani ni kiashiria cha kutapika nyongo. Hii ni kawaida kutokea kwa watu wanaotapika sana bila kuweka kitu tumboni na ni hali ya kawaida ambayo haipaswi kumwogopesha mtu.


Wakati gani wa kuwa na hofu unapotapika nyongo?


Endapo unatapika nyongo pamoja na dalili zifuatazo unapaswa kutilia mashaka na kutafuta msaada wa daktari;

  • Kizunguzungu

  • Dalili za vidonda vua tumbo ( kiungulia, maumivu chembe ya moyo, maumivu wakati wa kula chakula n.k)

  • Kupumua kwa shinda

  • Kutapika nyongo kwa muda mrefu

  • Kutapika zaidi ya masaa 48 bila kupata nafuu

  • Kutapika kila kitu

  • Maumivu makali ya tumbo nay a ghafla

  • Kuwa na kisukari

  • Kuishiwa nguvu au kupata uchovu mkali

  • Kupata kizunguzungu au kuzimia

  • Maumivu makali ya kifua

  • Kutapika mara kwa mara katika mwaka

  • Damu kwenye matapishi au matapishi kuwa meusi au rangi ya unga wa kahawa

  • Maumivu makali ya kichwa na homa


Huduma ya kwanza kwa mtu anayetapika sana;


Hatua ya muhimu kuchukua endapo unatapika sana ni kufika hospitali ili kupatiwa matibabu kw akutundikiwa dripu, hii itasaidia rejesha kiwango cha madini na maji ulichopoteza.


Kama unatapika kwa kiasi na unaweza kunywa maji, fanya iwezekanavyo kunywa maji kiasi kidogo sana lakini mara kwa mara. Ukipata maji ya Oral au wengine huita ORS na hutumika kwa watoto wanaoharisha itasaidia kuwa kama huduma ya kwanza. Kengo ni kurejesha kiwango ulichopoteza kwa kutapika na kuzuia kupata shoku kutokana na kuishiwa maji mwilini.


Zuia kutumia vitu vinavyokuletea kichefuchefu kama vinywaji nyenye mafuta, sukari na viungo kwa wingi na vingine ambavyo vinaamsha kuchefuchefu chako.


Rejea za mda hii


  1. Vomiting in adults. https://www.nhsinform.scot/illnesses-and-conditions/stomach-liver-and-gastrointestinal-tract/vomiting-in-adults. Imechukuliwa 28.06.2021

  2. Catiele Antunes, et al. Upper Gastrointestinal Bleeding. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK470300/#: Imechukuliwa 28.06.2021

  3. I.Dodd Wilson. Chapter 85Hematemesis, Melena, and Hematochezia. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK411/. Imechukuliwa 28.06.2021

  4. Amyloidosis. my.clevelandclinic.org/health/diseases/15718-amyloidosis. Imechukuliwa 28.06.2021

  5. Cyclic vomiting syndrome. niddk.nih.gov/health-information/digestive-diseases/cyclic-vomiting-syndrome. Imechukuliwa 28.06.2021

  6. Lamps LW, et al.Fungal infections of the gastrointestinal tract in the immunocompromised host: An update. DOI: 10.1097/PAP.0000000000000016. Imechukuliwa 28.06.2021

  7. Mayo Clinic Staff. Acute liver failure. mayoclinic.org/diseases-conditions/acute-liver-failure/symptoms-causes/syc-20352863. Imechukuliwa 28.06.2021

  8. Mayo Clinic Staff. Viral gastroenteritis (stomach flu). https://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/viral-gastroenteritis/symptoms-causes/syc-20378847. Imechukuliwa 28.06.2021

  9. Mayo Clinic Staff.Food poisoning. mayoclinic.org/diseases-conditions/food-poisoning/symptoms-causes/syc-20356230. Imechukuliwa 28.06.2021

  10. Mayo Clinic Staff.Gastritis.mayoclinic.org/diseases-conditions/gastritis/symptoms-causes/syc-20355807. Imechukuliwa 28.06.2021

  11. Mayo Clinic Staff.Gastroesophageal reflux disease (GERD). mayoclinic.org/diseases-conditions/gerd/symptoms-causes/syc-20361940. Imechukuliwa 28.06.2021

  12. Mayo Clinic Staff.Intestinal obstruction. mayoclinic.org/diseases-conditions/intestinal-obstruction/symptoms-causes/syc-20351460. Imechukuliwa 28.06.2021

  13. Mayo Clinic Staff.Nausea and vomiting. mayoclinic.org/symptoms/nausea/basics/definition/sym-20050736. Imechukuliwa 28.06.2021

  14. Mayo Clinic Staff.Vomiting blood. mayoclinic.org/symptoms/vomiting-blood/basics/definition/sym-20050732

  15. Nausea and vomiting in adults. nhs.uk/conditions/nausea-and-vomiting-in-adults/. Imechukuliwa 28.06.2021

  16. Nausea and vomiting. my.clevelandclinic.org/health/symptoms/8106-nausea--vomiting. Imechukuliwa 28.06.2021

  17. Vomit looks like coffee grounds after drinking alcohol. goaskalice.columbia.edu/answered-questions/vomit-looks-coffee-grounds-after-drinking-alcohol. Imechukuliwa 28.06.2021

  18. Vomiting in adults. (2018). nhsinform.scot/illnesses-and-conditions/stomach-liver-and-gastrointestinal-tract/vomiting-in-adults. Imechukuliwa 28.06.2021

684 Views

Kuhusu kundi

Uliza swali pamoja na kusoma majibu ya maswali yaliyoulizwa,...

bottom of page