top of page

Majadiliano na Wataalamu

Public·804 members

Kutokwa na ute mweupe mzito ukeni ni dalili ya mimba?

Ni kawaida mwanamke kutokwa na ute mweupe usio na harufu au wenye harufu kiasi kabla na wakati wa ujauzito. Hali ya kutokwa na ute huongezeka wakati wa ujauzito kutokana na ongezeko la homoni estrojeni kwenye damu inayotoa maelekezo ya kuongeza uzalishaji wa ute huu ukeni.


Aidha kutokwa na ute ukeni si tu kunaweza maanisha uwepo wa mimba, bali unaweza maanisha mwanamke anaingia kwenye kipindi cha uovuleshaji endapo hana mimba. Kipindi cha uovuleshaji ni kipindi cha hatari kushika mimba kinachodumu kwa masaa 24 hadi 36. Mwanamke akishiriki ngono wakati huu anaweza kubeba ujauzito.

 

Sifa za ute mweupe ulio kawaida wakati wa ujauzito

Mara nyingi huwa mweupe kama maji au karatasi

  • Hauna harufu au kuwa na harufu kiasi

  • Awali huwa mzito na baadae huwa mwembamba

  • Huongezeka ujauzito unavyokuwa

 

Ute mweupe wakati wa uovuleshaji

Huwa na sifa zifuatazo

  • Mweupe

  • Huwa mzito awali na baadae huwa mwembamba na kuteleza

  • Huweza kuonekana na weupe wa ute wa yai

  • Huwa hauna harufu

  • Huwa hauleti bugudha

 

Dalili nyingine za mimba

Dalili zingine za ujauzito ni pamoja na;

  • Kutokwa damu

  • Mabadiliko ya chuchu kama kuvimba, na kuuma

  • Kichefuchefu na kutapika

  • Kutoingia mwezini

  • Kutokwa matone ya damu

  • Mumivu ya tumbo la chini

  • Hisia za uchovu

 

Je, unathibitishaje kuwa una mimba?

Ili kuthibitisha kuwa una ujauzito, unapaswa kufanya vipimo. Kwa wiki za awali, vipimo vya sasa vya mkojo huwa havionyeshi uwepo wa mimba, hivyo utabidi kufanya ultrasound ya uke, au kipimo cha Homoni ujauzito kwenye damu. Endapo kipimo cha ultrasound kitafanyika na mtaalamu, ataweza kuona dalili za uwepo wa mimba. Endapo hakuna vipimo hivi, utabidi kusubiria wiki mbili zipite baada ya kushiriki ngono ili ufanye kipimo cha mimba cha kutumia mkojo.


Kumbuka

Wasiliana na daktari wako wakati wote uonapo dalili ambazo huzielewi kwa uchugnuzi na tiba na usitumie maelezo haya kufanya maamuzi ya kimatibabu pasipo kuwasiliana na daktari wako.


Rejea za mada hii

  1. How much vaginal discharge is normal? (2024). https://www.plannedparenthood.org/blog/how-much-vaginal-discharge-is-normal. Imechukuliwa 17.11.2024

  2. ULY CLINIC. Dalili za ujauzito. https://www.ulyclinic.com/dalili-za-ujauzito . Imechukuliwa 17.11.2024

  3. ULY CLINIC. Dalili za ujauzito wa wiki moja. https://www.ulyclinic.com/dalili-za-ugonjwa/dalili-za-ujauzito-wa-wiki-moja. Imechukuliwa 17.11.2024

  4. Signs and symptoms of pregnancy. (2022).

  5. https://www.nhs.uk/pregnancy/trying-for-a-baby/signs-and-symptoms-of-pregnancy/. Imechukuliwa 17.11.2024

  6. Vaginal discharge. (2024). https://www.nhs.uk/conditions/vaginal-discharge/. Imechukuliwa 17.11.2024

  7. Vaginal discharge during pregnancy. (2022). https://www.pregnancybirthbaby.org.au/vaginal-discharge-during-pregnancy. Imechukuliwa 17.11.2024

4056 Views

Kuhusu kundi

Uliza swali pamoja na kusoma majibu ya maswali yaliyoulizwa,...

bottom of page