top of page

Majadiliano na Wataalamu

Public·804 members

Nikijisaidia haja kubwa baada ya kumaliza hutoka damu muda mwengine haja kubwa huwa na mchirizi wa damu. Ni nini kisababishi?


43 Views

Tatizo la damu kwenye kinyesi huweza kusababishwa na hali au magonjwa mbalimbali ikiwepo  Bawasili(bonyeza kusoma), Kuhara, saratani ya utumbo mpana na matatizo mengine.

Mtu anaweza kuwa na damu inayoonekana nyekundu, nyeusi, au nyekundu iliyoganda. Lakini pia mtu anaweza kutoa mabonge ya damu wakati wa kujisaidia bila kutoa kinyesi. Dalili hizi mbalimbali husababishwa na sababu aina tofauti tofauti

Kutokwa na damu nyeusi wakati wa kujisaidia kunaweza kumaanisha damu imevuja mfumo wa juu wa tumbo kuanzia kwenye maeneo ya mrija wa esofagasi, tumbo la chakula, utumbo mwembamba na sehemu ya utumbo mpana. Hata hivyo endapo mtu anatoka kiasi kukubwa cha damu kwenye maeneo haya damu nyekundu inaweza kuonekana kwenye kinyesi ikiwa pamoja na mchanganyiko w akinyesi cheusi.


Soma zaidi makala hii kwa kubonyeza hapa

Kuhusu kundi

Uliza swali pamoja na kusoma majibu ya maswali yaliyoulizwa,...

bottom of page