top of page

Majadiliano na Wataalamu

Public·804 members

Nimonia ni dalili ya UKIMWI?

Swali lililoulizwa ni, Je, mtu akiwa na nimonia ni kwamba ana ukimwi?


Majibu.



Nimonia
Nimonia

Si kweli UKIMWI hutambulika kwa kupima tu. Watu wazima na watoto wenye kinga dhaifu ya mwili huweza shambuliwa na vimelea mbalimbali wanaosababisha maradhi mbalimbali ikiwa pamoja na nimonia. Baadhi ya haki na magonjwa yanayoshusha kinga ya mwili yameorodheshwa hapa chini.


Hali na magonjwa yanayoshusha kinga ya mwili


Baadhi ya hali na magonjwa yanayoshusha kinga ya mwili ni:

  • Matumizi ya dawa zinazoshusha kinga ya mwili kama dawa jamii ya corticosteroid, dawa za kuua chembe za saratani

  • Saratani ya chembe za mfumo wa kinga ya mwili

  • Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi

  • Lishe duni(utapiamlo, kifadulo n.k)


Kwa maelezo zaidi waweza kusoma makala ya kushuka kwa kinga ya mwili kutokana na magonjwa mengine

80 Views

Kuhusu kundi

Uliza swali pamoja na kusoma majibu ya maswali yaliyoulizwa,...

bottom of page