top of page

Majadiliano na Wataalamu

Public·804 members

Uchafu ukeni baada ya kujifungua

Baada ya kujifungua, ni kawaida kwa mwanamke kutokwa na uchafu ukeni ambao huwa ni mchanganyiko wa ute wa kizazi, damu na masalia ya uzao wa mtoto na kondo la nyuma. Uchafu huu hubadilika rangi na harufu kwa jinsi kiasi cha damu kinavyopungua.




Kwa kawaida inachukua wastani wa siku 14 kwa uchafu kuisha, hata hivyo baadhi ya wanawawe inaweza kuchukua mpaka siku 21 na kuendelea. Mabadiliko ya rangi huanza kuwa nyekundu, kahawia, njano na baadae huwa na rangi ya ute wa kawaida.


Ratiba ya mabadiliko ya rangi ya uchafu

Uchafu ukeni hupitia hatua zifuatazo za mabadiliko ya rangi

  • Mabadiliko ya rangi: Kuanza nyekundu hudumu kwa siku 1 hadi 4

  • Rangi ya kahawia hudumu kwa kuda wa siku 5 hadi 9

  • Rangi ya njano inayodumu kuanzia siku ya 10 hadi 15


Wakati gani uwe na wasiwasi

Licha ya kutokwa na uchafu ukeni kuwa ni hali ya kawaida baada ya kujifungua, uonapo dalili zifuatazo unapaswa kupata ushauri wa daktari:

  • Homa

  • Uchafu kuwa na rangi ya kijani

  • Uchafu ukizidi wiki sita( siku 42)

  • Kuwa na harufu muozo

  • Maumivu makali ya tumbo la chini

  • Kizunguzungu

  • Mapigo ya moyo kwenda mbio

  • Rangi ya uchafu kuendelea kuwa nyekundu

  • Kuwa na mabonge kwa zaidi ya siku 3 za mwanzo

  • Kuhisi kitu kinatoka ukeni

  • Ute kuwa mwingi pasipo kupungua kwa jinsi siku zinavyoenda


Rejea za makala hii

  1. Science direct. Lochia. https://www.sciencedirect.com/topics/medicine-and-dentistry/lochia. Imechukuliwa 18.11.2024

  2. NHS. Your body after the birth. https://www.nhs.uk/pregnancy/labour-and-birth/after-the-birth/your-body/. Imechukuliwa 18.11.2024

  3. Postpartum Bleeding (Lochia): What's Normal and What's Not?https://www.whattoexpect.com/pregnancy/symptoms-and-solutions/postpartum-bleeding.aspx. Imechukuliwa 18.11.2024

  4. Romano M, et al. Postpartum period: three distinct but continuous phases. J Prenat Med. 2010 Apr;4(2):22-5. Sherman D, Lurie S, Frenkel E, Kurzweil Y, Bukovsky I, Arieli S. Characteristics of normal lochia. Am J Perinatol. 1999;16(8):399-402.

  5. Oppenheimer LW, et al. The duration of lochia. Br J Obstet Gynaecol. 1986 Jul;93(7):754-7.

  6. Chi C, et al. Puerperal loss (lochia) in women with or without inherited bleeding disorders. Am J Obstet Gynecol. 2010 Jul;203(1):56.e1-5.

298 Views

Kuhusu kundi

Uliza swali pamoja na kusoma majibu ya maswali yaliyoulizwa,...

bottom of page