top of page

Majadiliano na Wataalamu

Public·804 members

Kipimo cha kucheki mimba kinatoa majibu ndani ya siku au miez mingapi?


43 Views

Kipimo cha kucheki mimba au kipima mimba kwa njia ya mkojo chenye jina la 'urinary dipstic for pregnancy' huweza kutambua mimba ya kuanzia wiki mbili tu yaani siku 14.


Mimba chini ya wiki mbili haiwezi kutambuliwa kwa kipimo hiki, kuna vipimo vingine vinavyoweza kutambua mimba kabla ya wiki mbili kama vile kipimo cha serum HCG damu cha kinachopima kiwango cha Homoni HCG kwenye damu, homoni ambayo huanza kuonekana kwenye mkojo wiki mbili baada ya ujauzito kutungishwa, na huweza kutambuliwa kwenye damu mapema zaidi kabla ya wiki mbili kwa kipimo hicho.


Mbali na vipimo hivi vya damu, kipimo cha picha ya Ultrasound pia kinaweza kutumika kutambua mimba chini ya wiki moja. Utahitaji kupimwa na mtu mzoefu ili kutambua ujauzito chini ya wiki moja.


Endapo una maswali zaidi wasiliana nadaktari wa ULY CLINIC au wasilisha swali lako kwenye tovuti kisha utajibiwa. Rejea siku zote kwa maboresho ya majibu kulingana na tafiti zilizofanyika

Kuhusu kundi

Uliza swali pamoja na kusoma majibu ya maswali yaliyoulizwa,...

bottom of page