top of page

Majadiliano na Wataalamu

Public·804 members

Dalili za typhoid kwa mwanamke


Dalili za typhoid kwa mwanamke ni zipi?


Watu wengi wamekuwa wakiuliza kuhusu dalili za taifodi kwa wanawake. Makala hii imelenga kujibu swali hili.


Dalili za typhoid kwa mwanamke hazitofautiani na wanaume, mgonjwa anaweza mwenye maambukizi ya taifoid au parataifodi mara nyingi huwa na homa endelevu inayoanza taratibu na kuongezeka siku zinavyoenda bila kupungua na huweza kufika nyuzi joto za sentigredi 39 au 40 pamoja na dalili zifuatazo;


  • Uchovu mkali wa mwili

  • Maumivu ya kichwa

  • Kuharisha au haja ngumu

  • Kikohozi kikavu

  • Kutokwa na jasho

  • Kupoteza hamu ya kula

  • Kupoteza uzito

  • Mabaka kwenye ngozi yenye rangi ya ua waridi (Angalia picha)


Wakati gani uonane na daktari unapokuwa na dalili za taifodi?


Mwone daktari haraka iwezekanavyo unapohisi kuwa una dalili za taifodi kwa uchunguzi na tiba


Majina mengine ya dalili za typhoid kwa mwanamke


Majina mengine yanayotumika kumaanisha dalili za typhoid kwa mwanamke ni;


  • Dalili za taifodi kwa mwanamke

  • Dalili ya taifod kwa mwanamke

  • Dalili ya homa ya matumbo kwa wanawake


Rejea za mada hii;


  1. CDC. Symptoms and Treatment. https://www.cdc.gov/typhoid-fever/symptoms.html. Imeandikwa 2.07.2021

  2. Jameson JL, et al. Salmonellosis. In: Harrison's Principles of Internal Medicine. 20th ed. McGraw Hill; 2018. https://accessmedicine.mhmedical.com. Imeandikwa 2.07.2021

  3. Ryan ET. Epidemiology, microbiology, clinical manifestations, and diagnosis of typhoid fever. https://www.uptodate.com/contents/search. Imeandikwa 2.07.2021

  4. ULY CLINIC taifodi

4572 Views

Kuhusu kundi

Uliza swali pamoja na kusoma majibu ya maswali yaliyoulizwa,...

bottom of page