Maambukizi ya virusi vya UKIMWI yanaweza kutambuliwa kwa vipimo mbalimbali kuanzia masaa 24 hadi hadi siku 90 baada ya kupata maambukizi. Vipimo maarufu vilivyopo ni;
Kipimo cha HIV DNA PCR, ambacho hutambua maambukizi ndani ya masaa 24. Kipimo hiki hupima nakala ya DNA ya kirusi kwenye damu na huwa na uwezo wa kutambua kuwepo kwa kirusi kwa asilimia 90 hadi 95. Kipimo cha HIV DNA PCR ni nadra kufanyika kwa sababu ya gharama zake na hakifanyiki bure.
vipimo vingine ambavyo hutumika sana kupima maambukizi ya VVU ni
Kipimo cha HIV antibody/antigeni test kinachofanyika maabara . Kipomo hiki hupima kiwango cha kemikali za ulinzi zinazozalishwa na mwili kuitikia maambukizi ya VVU zenye jina la antibody. Endapo damu ya kidole itatumika kupimwa na kipimo hiki, maambukizi yanaweza kugunduliwa kuanzia siku 19 hadi 90 ya kupata maambukizi, na endapo damu ya mishipa itatumika, maambukizi yatagunduliwa kuanzia siku 19 hadi 45 ya kupata maambukizi.Kipimo hiki huwa na uwezo wa kutambua maambukizi kwa asilimia 95.
Kipimo cha HIV antobody test, hutumia kit ya HIV SD bioline. Kipimo hiki hutambua kemikali za kinga mwilini zenye jina la antibody, ambazo huzalishwa kupambana na virusi vya UKIMWI. Kipimo hiki hufanyika kwenye vituo vya ushauri nasaa pamoja na hospitali, huwa na uwezo wa kutambua maambukizi ya VVU kuanzia siku 23 hadi 90 baada ya kupata maambukizi. Kipimo hiki huwa na uwezo wa kutambua maambukizi kwa asilimia 95.
Kuna baadhi ya watu hutumia kipimo cha Unigold ambacho kazi yake ni kuthibitisha endapo Kiti ya SD bioline imesoma HIV positive.
Kuhusu kundi
Uliza swali pamoja na kusoma majibu ya maswali yaliyoulizwa,...