top of page

Majadiliano na Wataalamu

Public·804 members

Kubeba ujauzito baaada ya kutumia Norethisterone

Maswali ya msingi


  1. Ni wakati gani mwanamke atabeba ujauzito baaada ya kutumia dawa ya Norethisterone?

  2. Je ni wakati gani utabeba ujauzito baada ya kuacha kutumia norethindrone


Majibu

Kushika mimba baada ya kuacha Norethisterone

Dawa Norethisterone ni homoni ya projestini inayotumika kwa hali na magonjwa mbalimbali, ikiwemo kuchelewesha hedhi, kutibu matatizo ya hedhi, na kama sehemu ya vidonge vya uzazi wa mpango. Ikiwa mwanamke ametumia Norethisterone kwa muda mfupi kama vile kwa kuchelewesha hedhi, uwezo wa kushika mimba unaweza kurejea haraka baada ya kuacha dawa.


Muda wa kushika mimba baada ya kuacha Norethisterone


Ikiwa ilitumiwa kwa kuchelewesha hedhi 

Mzunguko wa hedhi kwa kawaida hurejea ndani ya siku chache baada ya kuacha kutumia dawa, hivyo uovuleshaji unaweza kutokea katika mzunguko unaofuata. Mwanamke anaweza kushika mimba hata ndani ya wiki chache baada ya kuacha kutumia dawa.


Ikiwa ilitumiwa kwa matibabu ya muda mrefu

Ikiwa mwanamke ametumia Norethisterone kwa muda mrefu mfano kama sehemu ya matibabu ya hedhi zisizo za kawaida, inaweza kuchukua muda mrefu zaidi kwa mwili kurejea kwenye mzunguko wa kawaida wa hedhi na uovuleshaji. Tafiti zinaonyesha inaweza kuchukua wastani wa wiki 12 hadi miezi 6 kushika ujauzito baada ya kuacha dawa huku wengine wakichukua hadi mwaka mzima kwa mzunguko wa hedhi kurudi katika hali yake ya kawaida na kushika.


Jinsi ya kupima uwezekano wa kupata ujauzito


Ikiwa mwanamke anayetaka kushika mimba baada ya kuacha kutumia Norethisterone, anaweza kutumia vipimo vya uovuleshaji ili kujua wakati wa siku za hatari. Ikiwa hedhi haijarudi ndani ya wiki 4-6 baada ya kuacha dawa, inapendekezwa kufanya kipimo cha ujauzito au kushauriana na daktari.


Hitimisho

Kwa wanawake wengi, uwezo wa kushika mimba hurudi haraka baada ya kuacha kutumia Norethisterone na wanaobakia, inaweza kuchukua hadi miezi 12. Hii ni kulingana na mwitikio wa mwili wa mtu, madhumuni ya kutumia dawa na sababu zingine za kiafya.


Rejea za mada hii


  1. Royal College of Obstetricians and Gynaecologists (RCOG). Norethisterone for the Delay of Menstruation. Available at: https://www.rcog.org.uk. Imechukuliwa 01.04.2025

  2. National Library of Medicine (NLM), DailyMed. Norethisterone: Drug Information. Available at: https://dailymed.nlm.nih.gov/dailymed/drugInfo.cfm?setid=ccef4732-5307-7d4b-aa56-04aa6f2af5f9. Imechukuliwa 01.04.2025

  3. Mayo Clinic. Norethindrone (Oral Route) – Description and Precautions. Available at: https://www.mayoclinic.org/drugs-supplements/norethindrone-oral-route/description/drg-20137986. Imechukuliwa 01.04.2025

  4. British National Formulary (BNF). Progestogens: Norethisterone Uses and Side Effects. Available at: https://bnf.nice.org.uk/treatment-summary/progestogens.html. Imechukuliwa 01.04.2025

  5. MedlinePlus. Norethindrone: Medications and Usage. Available at: https://medlineplus.gov/druginfo/meds/a604032.html

  6. ULY Clinic. Matumizi ya Norethisterone na Athari Zake kwa Uzazi. Available at: https://www.ulyclinic.com/dawa/dawa-ya-norethisterone. Imechukuliwa 01.04.2025

  7. ULY Clinic.Ninaweza kupata mimba nikitumia norethisterone kuzuia kuingia piriodi kwa muda. Inapatikana: https://www.ulyclinic.com/majibu-ya-maswali/ninaweza-kupata-mimba-nikitumia-norethisterone-kuzuia-kuingia-piriodi-kwa-muda%3F. Imechukuliwa 01.04.2025

  8. Fotherby K, Yet al. Return of ovulation and fertility in women using norethisterone oenanthate. Contraception. 1984 May;29(5):447-55. doi: 10.1016/0010-7824(84)90018-0. PMID: 6744861.

34 Views

Kuhusu kundi

Uliza swali pamoja na kusoma majibu ya maswali yaliyoulizwa,...

bottom of page