Hofu na wasiwasi uliopitiliza
habari mi nilikuwa nina swali nimeona nakala yenu ya mwaka jana kama sikosei kuhusu hofu/ wasiwasi mm nina tatizo hilo yaan linanisumbua sana kila nikijitahid kujicontrol nashindwa inafika wakat natetemek hata nikiwa peke yangu sielew nikiwa kwa watu kabis hata kusimam siwezi. Hili tatizo linasababishwa na nini?
24 Views
Kila mtu hupata wasiwasi kwenye maisha yake, kuna mambo mengi yanayoweza kufanya mtu apate wasiwasi, mfano unapoenda kufanya mtihani, unapofanya interview ya kazi au unapowaza kuhusu kufanyiwa upasuaji. Wasiwasi ni kawaida kwenye maisha.
Hata hivyo hofu kwa watu wengi huja na kuondoka, endapo hofu inadumu hupelekea maisha yamtu kupungua thamani kwa kuishi bila kujiamini na kushindwa kushiriki vema kwenye kazi. Soma zaidi kwa kubonyeza hapa