top of page

Majadiliano na Wataalamu

Public·804 members

Homa ya njano

Homa ya njano husabaisha na nini?

11 Views

Homa ya manjano ni nini?

Homa ya manjano au homa ya njano ni ugonjwa unaosabababishwa na kirusi cha manjano. Unaweza pata maambukizi ya homa ya manjano endapo utang’atwa na mbu jike mwenye jina la anopheles aegypt na Haemogogus hasa kama unaishi Barani Afrika au umesafiri kwenda Amerika kusini.

Baada ya kung’atwa na mbu mwenye kirusi, inakadiliwa kuchukua siku 3 hadi 6 kabla ya kupata dalili na baada ya dalili kutokea itachukua siku 3 hadi 4 ugonjwa kupotea.


Dalili za wastani ya homa ya manjano ni zinajhusisha homa, maumivu ya kichwa, kichefuchefu na kutapika, baadhi ya watu hupata dalili kali zinazoashiria uhalibifu kwenye ogani mbalimbali ndani ya mwili kama moyo, ini na figo na damu. Wagonjwa wenye dalili kali asilimia zaidi ya 50 hufa na ugonjwa wa homa ya manjano.


Matibabu ya homa ya manjano hulenga kutibu dalili tu, endapo utaweza kupata chanjo pia ni vema maana utakuwa umepata kinga ya ugonjwa huu.


Dalili za homa ya njano


  • Homa

  • Maumivu ya kichwa

  • Maumivu ya misuli ya nyuma ya mgongo na magoti

  • Kuumizwa na mwanga

  • Kichefuchefu na kutapika

  • Kupoteza hamu ya kula

  • Kizunguzungu

  • Macho, uso na ulimi kuwa na rangi nyekundu


Dalili kali za homa ya njano


Watu wengi huishia kupata nafuu baada ya kupata dalili za wastani ndani ya siku 1 hadi 2. Hata hivyo badhi ya watu huendelea kwenye hatu a nyingine kali ya ugonjwa, ambapo hupata dalili kali zaidi zinazoashiria kuvunjwa vunjwa kwa chembe nyekundu za damu ambazo ni;


  • Manjano kwenye ngozi na macho

  • Maumivu ya tumbo

  • Kutapika na baadhi ya nyakati kutapika damu

  • Kupungua kwa kiasi cha mkojo

  • Kutokwa na damu puani, machoni na mdomoni

  • Mapigo ya moyo kwenda taratibu

  • Kuferi kwa ini na figo

  • Usingizi mkali kutokana na kuferi kwa ubongo

  • Degedege

  • Kupoteza fahamu


Kumbuka, homa ya njano ni tofauti na homa ya ini ( ambayo pia huwa na dalili ya manjano) na homa ya njano imeitwa jina hilo kutokana na mgonjwa kupata homa pamoja na kuwa na njano kwenye macho na ngozi. Kuna sababu nyingi pia zinazoweza pelekea mtu kupata njano, njano hizo huwa haziitwi kwa jina la homa ya manjano. Soma zaidi kuhusu makala hii ya homa ya njano kwa kubofya hapa au visababishi vingine vya homa ya manjano katika makala za tovuti ya ULY CLINIC au kwenye kipengele cha maswali yaliyoulizwa sana na majibu yake


Rejea za mada hii;


  1. Papadakis MA, et al. Common problems in infectious diseases & antimicrobial therapy. In: Current Medical Diagnosis & Treatment 2017. 56th ed. New York, N.Y.: McGraw-Hill Education; 2017. http://accessmedicine.mhmedical.com. Imechukuliwa 13.06.2021

  2. Monath TP. Yellow fever. http://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 13.06.2021

  3. Centers for Disease Control and Prevention. Yellow fever: Frequently asked questions. http://www.cdc.gov/yellowfever/qa/index.html. Imechukuliwa 13.06.2021

  4. Centers for Disease Control and Prevention .Protection against mosquitoes, ticks, & other insects & arthropods. http://wwwnc.cdc.gov/travel/yellowbook/2014/chapter-2-the-pre-travel-consultation/protection-against-mosquitoes-ticks-and-other-insects-and-arthropods. Imechukuliwa 13.06.2021

  5. Yellow fever. https://www.who.int/news-room/fact-sheets/detail/yellow-fever. Imechukuliwa 13.06.2021

Kuhusu kundi

Uliza swali pamoja na kusoma majibu ya maswali yaliyoulizwa,...

bottom of page