top of page

Majadiliano na Wataalamu

Public·804 members

je, unaruhusiwa kutumia erythromycin na fluconazole kwa pamoja?

Hapana!


Fluconazole huwa na mwingiliano na dawa mbalimbali ikiwa pamoja na warfarin, dawa za kunywa za kupunguza kiwango cha sukari kwenye damu, terfenadine, ergotamine, pimozide, dawa za asili na nyingine.


Fluconazole haipaswi kutumiwa pamoja na erythromycin. Hii ni kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuzuia vimeng'enya muhimu vya ini ambavyo hufanya umetaboliwa erythromycin ili kutoka mwilini. Fluconazole inaweza kuzuia umetaboli wa erythromycin mpaka siku 4 hadi 5 baada ya kumaliza dozi ya dawa. Hivyo inashauriwa kutotumia erythromycine mpaka siku 7 baada ya kumaliza dozi ya fluconazole.


Endapo utatumia dawa hizi mbili kwa pamoja, ni rahisi kupata maudhi makubwa/madhara ya erythromycin.


Rejea za mada hii;


  1. Drugs.com. Fluconazole vs erythromycin. https://www.drugs.com/tips/fluconazole-patient-tips. Imechukuliwa 10.05.2022

  2. Ray WA, Murray KT, Meredith S, Narasimhulu SS, Hall K, Stein CM. Oral erythromycin and the risk of sudden death from cardiac causes. N Engl J Med 2004 Sep 9;351(11):1089-96.

  3. Diflucan (fluconazole) US prescribing information. Pfizer Inc. March, 2020.

  4. Drew BJ, Ackerman MJ, Funk M, Gibler WB, Kligfield P, Menon V, Philippides GJ, Roden DM, Zareba W. Prevention of torsade de pointes in hospital settings: a scientific statement from the American Heart Association and the American College of Cardiology Foundation. J Am Coll Cardiol 2010 Mar 2;55(9):934-47.

  5. Phansalkar S, Desai AA, Bell D, Yoshida E, Doole J, Czochanski M, Middleton B, Bates DW. High-priority drug-drug interactions for use in electronic health records. J Am Med Inform Assoc 2012 Sep-Oct; 19(5):735-43.


14 Views

Kuhusu kundi

Uliza swali pamoja na kusoma majibu ya maswali yaliyoulizwa,...

bottom of page