top of page

Majadiliano na Wataalamu

Public·804 members

Mkojo harufu mbaya, vipele sehemu za siri|ULY CLINIC

Dokta, je kama mgonjwa anakojoa mkojo wenye harufu na anapata muwasho sehemu zote za siri pamoja na kutokwa vipele tatizo huwa nini?

35 Views

Harufu ya mkojo


Matumizi ya baadhi ya vyakula na dawa mfano baathi ya vitamin huweza kubadili harufu ya mkojo, hata hivyo kuwa na maji kidogo mwilini na maambukizi ya UTI pia huweza kubadili rangi pamoja na harufu ya mkojo


Sababu zingine zinaweza kuwa


  • Fistula kati ya mrija wa mkojo na njia ya haja kubwa

  • Kisukari aina ya pili

  • Ugonjwa wa maple syrup

  • Magonjwa ya kimetaboliki


Ili kujua zaidi kuhusu ni nini shida yako wasiliana na daktari wako kwa uchunguzi na Tiba.


Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba popote ulipo kwa kutumia namba za simu chini ya tovuti hii.

Kuhusu kundi

Uliza swali pamoja na kusoma majibu ya maswali yaliyoulizwa,...

bottom of page