top of page

Majadiliano na Wataalamu

Public·804 members

Kichomi husababishwa na nini?

Kichomi ni maumivu makali ya ghafla ya kifua, tumbo, misuli, mbavu n.k yanayodumu chini ya dakika moja. Maumivu haya huweza kuwa ya kuungua, kuchoma na kisu au mshale na yanaweza kutokea sehemu mbalimbali mwilini. Baadhi ya visabsbishi vya kichomi ni hali za kawaida na wakati mwingine huwa hali au magonjwa yanayohitaji matibabu ya kitabibu ya haraka. Makala hii imeelezea baadhi ya visababishi na matibabu yake.


Ni nini kinasabaibsha kichomi?

Visababishi vya kichomo ni vingi, makala hii imeelezea kisababishi vya kichomo haswa kichomi cha kifua. Kwa visababishi vya kichomi sehemu nyingine ya mwili, bofya linki zilizoorodheshwa kabla ya rejea za makala.


  1. Sindromu ya prekodio kachi (PCS)

Kisababishi: Hali isiyo na madhara ambayo huwapata zaidi vijana kutokana na kubanwa kwa neva kwenye kuta za kifua.


Dalili:

  • Maumivu makali ya kuchoma sehemu moja ya kifua

  • Yanadumu kwa sekunde chache hadi dakika moja

  • Huwa makali zaidi unapojaribu kupumua kwa kina


Matibabu:

  • Hakuna tiba inayohitajika; huisha yenyewe

  • Jaribu kupumua taratibu na kwa kina


2. Kukaza au kubana kwa misuli ya kifua

Kisababishi: Misuli ya kifua inaweza kukaza ghafla kutokana na mazoezi, mkao mbaya, au msongo wa mawazo.


Dalili:

  • Maumivu ya ghafla na makali kwenye sehemu fulani ya kifua

  • Huwa makali zaidi unapobadilisha mkao au kuhema kwa kina


Matibabu:

  • Mazoezi ya kunyoosha misuli na kupumzika

  • Weka kitambaa cha moto au baridi kwenye eneo lenye maumivu

3. Kucheua tindikali (GERD) au kubana kwa koo la chakula

Kisababishi: Tindikali ya tumbo inapopanda juu hadi kwenye koo la chakula, husababisha hisia ya kuungua au maumivu ya ghafla kwenye kifua.


Dalili:

  • Maumivu ya kuchoma au kuchoma yanayodumu sekunde chache

  • Huwa mbaya zaidi baada ya kula au kulala

  • Inaweza kufanana na maumivu ya moyo

Matibabu:

  • Chukua antacids (mfano: Omeprazole, Ranitidine)

  • Epuka vyakula vyenye mafuta mengi au viungo vikali

  • Usilale mara tu baada ya kula

4. Maumivu ya neva za mbavu

Kisababishi: Maambukizi au shinikizo kwenye neva zilizo kati ya mbavu, mara nyingi kutokana na vidonda vya neva au majeraha madogo.


Dalili:

  • Maumivu makali na ghafla kwenye mbavu au kifua

  • Huwa makali zaidi unapoinama au kuzunguka

Matibabu:

  • Dawa za kupunguza maumivu (Paracetamol, Ibuprofen)

  • Dawa za neva (mfano: Gabapentin ikiwa maumivu yanarudia)

5. Kostokoondraitiz (Uvimbekinga wa kifupa cha kifua)

Kisabaishi: Uvimbe kwenye kartileji inayounganisha mbavu na mfupa wa kifua (sternum).


Dalili:

  • Maumivu makali na ya ghafla kifua cha mbele

  • Yanakuwa mabaya zaidi unapobonyeza eneo hilo

  • Huathiri watu wa umri wote


Matibabu:

  • Dawa za kupunguza maumivu (Ibuprofen, Diclofenac)

  • Weka kitambaa cha moto kwenye eneo lenye maumivu


6. Wasiwasi au hofu kuu

Kisababishi: Wasiwasi mkubwa au msongo wa mawazo unaweza kusababisha kubana kwa kifua kwa ghafla kutokana na mwitikio wa homoni za woga kwenye misuli ya kifua.


Dalili:

  • Maumivu ya kifua ya muda mfupi

  • Mapigo ya moyo kwenda kasi

  • Kupumua kwa shida au kuhisi kizunguzungu


Matibabu:

  • Pumua polepole na taratibu

  • Jaribu kupumzika na kujituliza


Ni wakati gani uwasiliane na daktari haraka unapokuwa na kichomi?

Kama una kichomo na kinaambatana na dalili zifuatazo, onana na daktari haraka kwani dalili hizi zinaweza kuwa dalili za shambulio la moyo au tatizo lingine kubwa;

  • Kupumua kwa shida

  • Kizunguzungu au kuzimia

  • Maumivu kusambaa kwenye mkono, taya, au mgongo

  • Kutokwa na jasho jingi au kichefuchefu

  • Historia ya ugonjwa wa moyo


Wapi utapata maelezo zaidi kuhusu kichomi?

Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu visabishi vya kichomi katika maeneo mengine ya mwili kwa kubofya linki zinazofuata;


Rejea za mada hii

  1. ULY CLINIC. Kichomi cha kifua. https://www.ulyclinic.com/dalili-za-ugonjwa/kichomi-cha-kifua. Imechukuliwa 12.03.2025

  2. NHS. Pericarditis. nhs.uk/conditions/pericarditis/. Imechukuliwa 12.03.2025

  3. Health talk. Is your chest pain a sign of a heart attack, or something else?. healthtalk.unchealthcare.org/is-your-chest-pain-a-sign-of-a-heart-attack-or-something-else/. Imechukuliwa 12.03.2025

  4. Hsia RY, et al. A national study of the prevalence of life-threatening diagnoses in patients with chest pain.10.1001/jamainternmed.2016.2498. Imechukuliwa 12.03.2025

  5. Chest pain that isn’t caused by a heart attack.

  6. healthcare.utah.edu/the-scope/shows.php?shows=0_w2kx6v18. Imechukuliwa 12.03.2025

  7. Am I having a panic attack or a heart attack?. adaa.org/living-with-anxiety/ask-and-learn/ask-expert/how-can-i-tell-if-i%E2%80%99m-having-panic-attack-or-heart-atta. Imechukuliwa 12.03.2025

  8. Acid reflux.patients.gi.org/topics/acid-reflux/. Imechukuliwa 12.03.2025

  9. Myocarditis and Pericarditis Following mRNA COVID-19. https://www.cdc.gov/coronavirus/2019-ncov/vaccines/safety/myocarditis.html#. Imechukuliwa 12.03.2025

  10. Mayo Clinic. Myocarditis - Symptoms and causes - https://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/myocarditis/symptoms-causes/syc-20352539. Imechukuliwa 12.03.2025

88 Views

Kuhusu kundi

Uliza swali pamoja na kusoma majibu ya maswali yaliyoulizwa,...

bottom of page