top of page

Majadiliano na Wataalamu

Public·804 members

Kuwashwa uke

Miwasho sehemu za siri ni nini kisababishi?

Kuna sababu mbalimbali zinazoweza kusababisha muwasho ukeni. Watu wengi wamekuwa wakifahamu muwasho ukeni husababishwa na maambukizi ya fangasi tu, hii sio sahihi kwa kuwa kuna visababishi vingine vingi vinavyochangia. Tatizo la muwasho ukeni ni kubwa na hupelekea mwanamke kupatamatatizo ya kisaikolojia kwa kuwa mara nyingi inakuwa vigumu wakati mwingine kusema kwa daktari kwamba nina tatizo sehemu zangu za siri. Hata hivyo endapo una tatizo la kuwashwa ukeni, hupo peke yako na daktari anaweza kukusaidia kupata tiba rahisi itakayoondoa tatizo lako na kukupa uhuru zaidi na kujiamin.


Visababishi vya kuwashwa uke


Muwasho ukeni ni ishara ya mwitikio wa mwili kwenye maambukizi au kitu kigeni sehemu za siri. Visabaishi vinaweza kuwa;

  • Bakteria vajinosis

    • Huleta dalili ya muwasho pamoja na hisia za kungua , kutoa harufu mbaya kama samaki aliyeoza na kutoa uchafu ukeni wa rangi tofauti




  • Mzio(allergy) na uchafu au manukato mbalimbali

    • Pedi za kutia ukeni ( tampoon)

    • Manukatoya kutia ndani ya uke

    • Nguo jamii ya nylon na polyester



Unawezaje kutambua kisababishi halisi cha muwasho uke?


Ili uweze kutambua kisababishi cha muwasho ukeni, unatakiwa kufahamu kuhusu sifa za magonjwa yaliyoandikwa haswa dalili zake na mwonekano wake na wakati mwingine unahitaji kuthibitisha kwa vipimo. Daktari wako anaweza kutambua kwa kuchukua historia yako na kufanya uchuguzi wa awali ukeni au kuagiza vipimo kufanyika.


Ufanye nini endapo una muwasho ukeni?


Endapo una muwasho ukeni, wasiliana na daktari wako kwa uchunguzi na tiba kabla ya kutumia dawa yoyote


Matibabu ya muwasho ukeni


Kwa sababu kuna visababishi vingi vya miwasho ukeni, baada ya daktari wako kuchukua historia ya tatizo lako na kukufanyia vipimo atakupa tiba kutokana na kisababishi. Dawa utakazopewa zinaweza kuwa za kupunguza dalili ya muwasho na dawa za kutibu maambukizi ukeni au dawa za kutibu maambukizi tu.


Dawa za kuficha muwasho ukeni


Dawa zifuatazo huficha muwasho ukeni lakini kamwe hazitibu kisababishi;

  • Krimu ya Hydrocortisone

  • Diphenhydramine

  • Benzocaine

  • Ciclosporin

  • Triamcinolone

  • Doxepin

  • Fluoxetine

  • Sertraline


Dawa za kutibu maambukizi


Endapo maambukizi ya fangasi ndo kisababishi, dawa za antifango zitatumika, zinaweza kuwa kati ya;

  • Terbinafine

  • Butenafine

  • Dawa ya kupaka ya Clotrimazole

  • Miconazole

  • Ketoconazole

  • Dawa ya kupaka ya Econazole

  • Luliconazole

  • Naftifine

  • Oxiconazole

  • Tolnaftate

  • Ciclopirox

  • Itraconazole

  • Sulconazole

  • Griseofulvin


Dawa hizi zinaweza kuwa za kupaka, kunywa au kidonge cha kuweka ukeni, utashauriwa na daktari ni dawa gani itakufaa kulingana na umri wako, hali ya ujauzito na ukubwa wa tatizo


Maambukizi ya vajinosisi ya bakteri


Hutibiwa kwa dawa za antibayotiki kama;


  • Metronidazole

  • Tinidazole


Maambukizi ya magonjwa ya zinaa ya bakteria


Magonjwa ya zinaa kama kisonono, kaswende na trikomoniasis yanayosababishwa na bakteri hutibiwa kwa dawa za antibayotiki kama vile;


  • Penicillin G

  • Azithromycin

  • Doxycycline

  • Ceftriaxone

  • Metronidazole

  • Tinidazole

  • Azithromycin

  • Cefixime

  • Cefotaxime

  • Ceftizome

  • Erythromycin

  • Gemifloxacin

  • Gentamicin


Soma zaidi kuhusu magonjwa ya zinaa na matibabu yake kwa kubofya hapa


Magonjwa ya zinaa ya virusi


Magonjwa ya zinaa kutokana na virusi hayana tiba ponyaji mpaka sasa, hata hivyo kuna dawa za kupunguza dalili za ugonjwa kwa kuzuia kuzaliana sana kwa virusi ambazo ni;


  • Inosine pranobex

  • Acyclovir

  • Famciclovir

  • Valaciclovir

  • Gancyclovir


Dawa asilia za muwasho ukeni


Kuna dawa za asili za muwasho ukeni unaweza kuandaa mwenyewe au kununua kutoka kwenye maduka mbalimbali ya dawa asilia, baadhi ya dawa hizo ni;



Namna ya kuthibiti na kujikinga na muwasho ukeni


Baadhi ya watu huwa na muwasho ukeni kwa sababu ya uchafu au matumizi ya vichokoza ngozi ukeni, vichokoza ngozi husababisha mzio wa ngozi ya uke. Huweza kuwa sabuni kali n.k endapo unawashwa uke, unaweza kutumia mbinu zifuatazo kama matibabu ya nyumbani ya kuwashwa uke;


  • Tumia maji ya kawaida kujiosha uke badala ya sababuni au vitakasa kusafishia uke. Uke una njia asili ya kujisafisha, na hauhitaji kutakaswa kwa sababuni au kemikali zozote

  • Tumia pedi za kawaida ambazo si za kuchomeka ndani ya uke

  • Vaa nguo za ndani zisizobana na haswa zilizotengenezwa na pamba. Nguo za nylon huleta joto ukeni na pia nyuzi zake huchokoza ngozi na kusababisha muwasho

  • Hakikisha unabadilisha nguo za ndani kwa wakati, usirudie nguo ile ile kila siku

  • Usiweke manukato ndani ya uke

  • Baada ya kushuriki ngono bila kinga, hakikisha unajisafisha kwa maji safi tu, isipokuwa endapo unataka kupata mimba

  • Tumia dawa za kupaka kama, Krimu ya Calcipotriene, Pimecrolimus au tacrolimus kwa magonjwa ya ngozi yanayosabaishwa na soriasis


Kudhibiti muwasho ukeni kutokana na magonjwa ya ngozi


Ili kudhibiti kuwashwa ukeni kutokana na magonjwa ya ngozi kabla ya kuonana na daktari wako unaweza kutumia njia zifuatazo;


  • Paka dawa za kununua duka la dawa muhimu jamii ya corticosteroid au antihistamine ili kuficha muwasho

  • Paka mafuta jamii ya petroleum(kama mafuta ya vasselin blue seal yasiyotiwa pafumu) au aquaphor

  • Safisha taratibu eneo lenye muwasho kilasiku na kausha, usitumie sabuni au manukato makali au kusafisha mara kwa mara

  • Ondoa hisia za kuungua kwa kutumia mafuta au kukalia maji ya uvuguvugu, barafu au kitambaa cha maji baridi

  • Zuia mkojo kugusa mashavu ya uke, baadhi ya magonjwa ya ngozi yanapoguswa na mkojo maumivu au muwasho huzidi zaidi mfano soriasis


Majina mengine yanayotumika kumaanisha tatizo la kuwashwa ukeni


Baadhi ya watu hutumia majina haya kumaanisha kuwashwa ukeni


  • Muwasho ukeni

  • Kujikuna ukeni

  • Kuungua ukeni

  • Kuungua uke

  • Kuwashwa uke

  • Kuwashwa mashavu ya uke

  • Kuwashwa ndani ya uke

  • Kujikuna mashavu ya uke

  • Dawa za muwasho ukeni

  • Dawa ya uke unaowasha


Rejea za mada hii


  1. Linn Woelber, et al. Vulvar Pruritus—Causes, Diagnosis and Therapeutic Approach. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC7081372/. Imechukuliwa 02.07.2021

  2. Julien Lambert. Pruritus in Female Patients. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3966341/. Imechukuliwa 02.07.2021

  3. ULY CLINIC. Maambukizi ya fangasi ukeni. https://www.ulyclinic.com/fungasi-ukeni. imechukuliwa 02.07.2021

  4. ULY CLINIC.Magonjwa ya zinaa. https://www.ulyclinic.com/magonjwa-na-saratani/Magonjwa-ya-zinaa. imechukuliwa 02.07.2021

  5. ULY CLINIC. Miwasho sehemu za siri-ukeni. https://www.ulyclinic.com/miwsho-ukeni. Imechukuliwa 02.07.2021

  6. Dawa za utibu gono. https://www.ulyclinic.com/dawa-gono. Imechukuliwa 02.07.2021

  7. ULY CLINIC. Dawa za kutibu herpes. https://www.ulyclinic.com/dawa-za-herpes-na-varicella-zoster. Imechukuliwa 02.07.2021

  8. ULY CLINIC. Dawa za kutibu fangasi maeneo ya siri. https://www.ulyclinic.com/dawa-za-kutibu-fungus-maeneo-ya-sir. Imechukuliwa 02.07.2021

  9. ULY CLINIC. Ngozi kuwasha. https://www.ulyclinic.com/kuwashwa-ngozi. Imechukuliwa 02.07.2021

  10. ULY CLINIC. Kuwawshwa pumbu na matibabu yake. https://www.ulyclinic.com/foramu/majadiliano-na-wataalamu/kuwashwa-sana-kwenye-pumbu-ni-dawa-gani-ya-kutumia. Imechukuliwa 02.07.2021

  11. American family physician. Vaginitis. https://www.aafp.org/afp/2018/0301/p321.html. Imechukuliwa 02.07.2021

  12. Mayo clinic. Lichen Sclerosis. https://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/lichen-sclerosus/diagnosis-treatment/drc-20374452. Imechukuliwa 02.07.2021

  13. Medical news. What to know about pephigoid. https://www.medicalnewstoday.com/articles/318015. Imechukuliwa 02.07.2021

  14. American Academy of dermatology asscociation. Howcan i treat genital soriasis. https://www.aad.org/public/diseases/psoriasis/treatment/genitals/genital-treat. Imechukuliwa 02.07.2021

7302 Views

Kuhusu kundi

Uliza swali pamoja na kusoma majibu ya maswali yaliyoulizwa,...

bottom of page