Mwandishi:
Dkt. Benjamin M, MD
Mhariri:
Dkt. Adolf S, MD
22 Machi 2020 13:22:27

Matibabu ya mikraruzo na majeraha madogo mwilini
Kila mtu ana Kihatarishi cha kupata majeraha madogo kwenye Ngozi kwa kujikata au kukwaruzwa na kitu au kuanguka. Wakati mwingine unapopatwa na tatizo hili unaweza kuwa na hofu ya nini kitakachotokea baada ya majeraha hayo. Sehemu hii imezungumzia kuhusu matibabu ya nyumbani ya majeraha madogo.
Majeraha madogo kwenye Ngozi ni nini?
Aina za majeraha kwenye Ngozi yanaweza kuwa ni majeraha madogo ambayo hayajazama ndani ya Ngozi au majeraha yaliyozama ndani.
Majeraha ambayo hayajazama ndani ni kama vile;
Mikraruzo kwenye Ngozi, abrasheni, kuungua kwa Ngozi ya juu. Mikraruzo hutokea sana kwenye magoti kiwiko cha mkono na viganja vya mikono. Huweza kutokana na kuanguka wakati mtu anatembea au kukimbia.
Majeraha ambayo yamezama ndani Zaidi
Mareraha ya kukatwa na kitu chenye ncha kali, lasalesheni, na kusagika kwa Ngozi
Jeraha la bruizi
Wakati gani unahitaji matibabu ya kushonywa na nyuzi unapokuwa na majeraha kwenye ngozi?
Jeraha lolote lile ambalo limepasua Ngozi na kuzama Zaidi ya milimita 12 kwenye Ngozi linahitaji kushonwa ili lisipone kwa kuleta kovu kubwa
Michaniko kwenye uso Zaidi ya milimita 6 inahitaji kushonwa pia
Kidonda chochote kinachohitaji matibabu ya kushonywa kinatakiwa kionwe mapema iwezekanavyo na daktari ikiwezekana ndani ya masaa sita toka jeraha limetokea. Malengo ni kuzuia maambukizi yasitokee kwenye kidonda maana yanaweza kubadili matibabu
Je unajuaje hili ni jeraha la mkraruzo au la kukatwa?
Ni muhimu ukiwa unaamua kutibu majeraha madogo ukatathmini mambo yafuatayo.
Ngozi ya binadamu ina upana wa milimita 3
Majeraha ya kujikata na lasaresheni hukata upana huu wote
Mikraruzo huwa mara nyingi haimalizi upana wote wa ngozi
Majeraha ya kujikata ambayo yanaweka uwazi wakati wa mjongeo yanahitaji kushonwa ili kuzuia kupona kunakoambatana na makovu
Mikraruzo na majeraha yanayofanana nayo mara nyingi huwa hayahitaji kushonwa hata yakiwa yamedhuru eneo kubwa kiasi gani
Wakati gani wa kuwasiliana na daktari?
Ukiwa na majeraha ya ngozi, mpigie daktari wako haraka kwa huduma ya kwanza endapo;
Ngozi imekatwa na ina hitaji kushonwa
Maumivu makali kuendelea masaa mawili baada ya kutumia dawa za maumivu
Kuwa na umri chini ya mwaka mmoja
Kuna uchafu kwenye kidonda hata baada ya kujisafisha na maji safi
Ngozi imeraruka
Mikraruzo iliyo athiri sehemu kubwa ya mwili
Mikraruzo au majeraha ya kujikata yanayoonekana kuwa yana maambukizi (kuwa mekundu, kutoa
usaha)
Kama umejikata na hujapata chanjo ya tetenasi au chanjo imeisha muda wake
Kama unafikiria una jeraha kubwa
Kuwa na bruizi kubwa licha ya kuwa na jeraha dogo sana
Bruizi kutokea bila jeraha lolote
Kidonda hakiponi licha ya siku 10 kupita
Una maswali mengine au unahitaji ushauri
Matibabu ya nyumbani ya mikwaruzo kwenye ngozi
Matibabu ya majeraha ambayo hayajazama chini ya Ngozi
Tumia nguvu kiasi kugandamiza maeneo hayo ili yasiendelee kuvuja damu, fanya hivi kwa dakika 10 mpaka damu itakapoacha kutoka
Osha eneo lililoathirika kwa kutumia maji yanayotiririka kwa muda wa dakika 5
Tahadhari- usiloweke eneo ambalo litahitaji kushonwa maana litavimba na kusababisha lisiweze kushonwa kirahisi
Tumia tauro safi isiyoacha nyuzunyuzi ili kuondoa uchafu kwenye kidonda endapo hautoki kwa kuosha tu
Tumia dawa ya antibayotiki ya kupaka kama vile polysporin kutoka kwenye maduka ya dawa baridi. Au mpigie daktari wako akuandikie. Baada ya kupaka hakikisha unafunika eneo na bandeji mpya. Na fanya ivi kila siku
Matibabu ya Majeraha madogo ya kujikata
Tumia dandeji tepe kufunika kidonda. Hii inaweza kufunika kidonda kwa muda wa wiki moja tu
ukilinganisha na badeji zingine ambazo zinatakiwa kubadilishwa kila siku, pia huchochea kupona kwa kidonda haraka na kuzuia maambukizi.
Matibabu ya bruizi
Matibabu ya bruizi hayajaongelewa hapa ila yameongelewa sehemu nyingine kwenye tovuti hii
Dawa za maumivu mtu mwenye majeraha kwenye ngozi
Ili kuondoa maumivu unahitaji kutumia dawa za kupunguza maumivu kama vile parasetamo au ibrupofen.
Ingia kwenye mada ya dawa za maumivu kusoma Zaidi kuhusu dawa za kupunguza maumivu.
Chanjo ya tetenasi kwa mgonjwa mwenye majeraha kwenye ngozi
Unatakiwa kupata chanjo endapo chanjo ya tetenasi uliyopewa tayari imeisha muda wake
Soma zaidi kwenye Makala zetu muda gani chanjo ya tetenasi hudumu mwili na wakati gani unatakiwa kupata chanjo nyingine.
Kwa vidonda ambavyo vimesababishwa na vitu vichafu au kupatwa na uchafu wakati wa kupata jeraha unatakiwa kupigwa chanjo ya tetenasi ili kubusti endapo miaka mitano imeshapita toka upate chanjo ya mwisho.
Kwa kidonda kisafi au ambacho kimesababishwa na kitu kisafi kisicho na kutu au mchanga, utatakiwa kupata chanjo ya kubusti ya tetenasi endapo muda umeshapita miaka kumi tokea upate chanjo ya mwisho.
Lini kidonda kitapona?
Kwa vidonda vidogo vya kujikata au kukwaruza kidonda kitapona ndani ya muda wa wiki moja
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasilianane na daktari wako kwa ushauri zaidi na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote baada ya kusoma makala hii
Wasiliana na daktari wa ULY clinic kwa kupiga namba za simu au kubonyeza sehemu imeandikwa "Pata tiba" chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
21 Julai 2023 16:20:09
Rejea za mada hii;
1. Bailey & Love's Short Practice of Surgery, chapisho la 27
2. American College of Emergency Physicians Foundation: "Cuts and abrasions."