Mwandishi:
Dkt. Benjamin M, MD
Mhariri:
Dkt. Mangwella S, MD
23 Machi 2020 16:46:35
Matibabu ya maumivu ya Kichwa
Kila mtu anaweza kuwa ashawahi pata maumivu ya kichwa katika Maisha yake. Wakati mwingine unaweza kujiuliza sababu ni nini husababisha maumivu haya? Na wakati mwingine ukawa na hofu kuhusu nini kitatokea baada ya maumivu hayo
Kitiba, maumivu ya kichwa yanaweza kusababishwa na sababu nyingi zikiwa pamoja na matatizo kwenye ubongo, mishipa ya damu, mishipa ya fahamu, fuvu la kichwa, misuli ya kichwani na pia kuna baadhi ya watu wamerithi tatizo la maumivu ya kichwa linalotembea katika familia.
Maumiu ya kichwa pia yanaweza kusababishwa na vitu vya hatari au visivyo vya hatari, unahitaji kuwasiliana na daktari wako sikuzote kwa ushauri hata kama utakuwa unachukua jitihada za kupunguza maumivu hayo
Baadhi ya matibabu ya maumivu ya kichwa ukiwa nyumbani ni pamoja;
Kujikanda na maji ya baridi au barafu kutibu maumivu ya kichwa
Tumia taulo lililochovya kwenye maji ya baridi au barafu kukanda eneo la paji la uso ili kupunguza maumivu
Gandamiza kwa muda wa dakika 10 hadi 20 baada ya hapo pumzika kwa muda wa dakika 10 hadi 15 kabla ya kurudia tena mara nyingine. Unaweza kufanya hivi mara nyingi unavyoweza
Zuia vitu vinavyobana kichwani kutibu maumivu ya kichwa
Regeza nguo au kofia zinazobana kichwa, nguo zinazobana kichwa zinaweza kusababisha maumivu ya kichwa kwa kuleta mgandamizo. Pia kusuka mitindo ya nywele za kuvuta sana kichwa huweza kusababisha maumivu ya kichwa
Punguza kupigwa na mwanga machoni kutibu maumivu ya kichwa
Mwanga mkali unasemekana kuamsha maumivu ya kichwa ya kipanda uso, hivyo ni vema kufanya yafuatayo ili kupugnuza mwanga mkali kwenye macho yako;
Acha kuangalia mwanga wenye kimulimuli, punguza mwanga wa kompyuta yako kama unatumia kompyuta au tumia mode ya kusomea
Weka kipunguza mwanga kwenye kioo cha kompyuta yako ili kuzuia mwanga mkali kupiga kwenye macho yako
Unapokuwa upo nje ya nyumba tumia miwani ya kupunguza mwanga wa jua
Acha kutafuna tafuna vitu kuzuia maumivu ya kichwa
Kutafuna bablishi au vitu vigumu licha ya kuleta maumivu kwenye taya, husababisha maumivu ya kichwa pia, acha kutafuna kucha za vidole
Kama unatabia ya kutafuna meno wakati wa usiku unaweza kutumia grili za meno ili kuzuia hali hii .
wasilaina na daktari wako wa meno kwa msaada zaidi
Kunywa chai asubuhi kama tiba ya maumivu ya kichwa
Tumia chai ya moto yenye kahawa asubuhi na mapema unapoamka, kufanya hivi husaidia kupunguza maumivu ya kichwa. Usitumie kahawa nyingi sana kwa sababu mara utakapoacha matumizi ya kahawa maumivu yatakuja mara dufu.
Chai ya tangawizi katika tafiti inaonekana pia kupunguza maumivu ya kichwa kwa watu wenye kipanda uso, unaweza kutumia chai ya tangawizi kwa jinsi unavyoweza ili kupunguza maumivu ya kichwa
Fanya mazoezi kama tiba ya maumivu ya kichwa
Fanya mazoezi ya mwili na yoga pamoja na kufanya meditesheni. Jifunze Zaidi kuhusu mazoezi kwenye sehemu ya mazoezi na chakula katika tovuti hii.
Mwombe daktari wa mazoezi pia akufundishe namna ya kupambana na maumivu kwa kukuelekeza aina ya mazoezi ya kufanya
Fanya maseji kwenye maneo haswa ya taya la juu na kichwani ili kupunguza maumivu ya kichwa
Usipende matumizi sana ya dawa za maumivu kutibu maumivu ya kichwa
Tumia maji badala ya dawa za maumivu
Ongea na daktari wako kuhusu matumizi ya dawa za maumivu kwa sababu baadhi ya dawa zinazotumiwa huweza kusababisha vidonda vya tumbo na matatizo mengine endazo zinatumika mara kwa mara na baadhi ya dawa hazipaswi kutumika kwa sababu zinaweza kuleta maumivu Zaidi ya kichwa
Acha kutumia pombe kuzuia maumivu ya kichwa
Matumizi ya pombe yanaweza kuambatana na maumivu ya kichwa wakati wa asubuhi kama hang’ova
Acha kutumia pombe kwa kiasi kikubwa au acha kabisa endapo unapata maumivuu baada ya kutumia pombe
Jaribu kutafuta mbadala wa kinywaji hiki kwa kutumia maji au kufanya mazoezi
Endapo itabidi, tumia aina nyingine ya pombe ambayo zinafahamika kutosababisha hang’ova
Tahadhari unashauriwa kutumia kiasi cha pombe kinachofaa kiafya, soma kuhusu kiasi gani cha pombe kinafaa kiafya katika makala sehemu nyingine katika tovuti hii
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasilianane na daktari wako kwa ushauri zaidi na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote baada ya kusoma makala hii
Wasiliana na daktari wa ULY clinic kwa kupiga namba za simu au kubonyeza sehemu imeandikwa "Pata tiba" chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
21 Julai 2023 16:20:09
Rejea za mada hii;
1.Beth Israel Deaconess Medical Center: "Have a Headache at Work? 13 Quick Fixes." National Headache Foundation: "Hot and Cold Packs/Showers."
2.National Health Service (UK): "Sinus headache." Blau, JN. Headache, published online May 2004.
3.The International Headache Classification ICHD-2: "External Compression Headache."
4.Mount Sinai Hospital: "Managing Your Migraines"
5.National Health Service (UK): "10 Headache Triggers."
6.National Headache Foundation: "Bruxism." American Headache Society: "Dental Appliances and Headache."
7.The Migraine Trust: "Medication for Migraine." American Headache Society: "Acute Therapy: Why Not Over-The-Counter or Other Nonspecific Options?"
8.American Headache Society: "Ten Things That You and Your Patients with Migraine Should Know." Lawrence C. Newman, MD, President, American Headache Society and Director, Headache Institute, Mount Sinai Roosevelt Hospital, New York City.
9.American Academy of Neurology: "Migraine Headache."
10.American Migraine Foundation: "Headache Hygiene - What is it?"
11.American College of Physicians: "Managing Migraine."
12.Johns Hopkins Medicine: "Chronic Daily Headache."
13.Mayo Clinic: “Acupuncture,” “Migraine,” “Migraines: Simple steps to head off the pain,” “Rebound headaches,” “Tension headache.”
14.Cleveland Clinic: “Self-Care Treatments for Headaches: Procedure Details.”
15.National Center for Complementary and Integrative Health: “Acupuncture: In Depth,” “Butterbur,” “Feverfew.” Cephalalgia: “Double-blind placebo-controlled randomized clinical trial of ginger (Zingiber officinale Rosc.) addition in migraine acute treatment.”
15.Phytotherapy Research: “Comparison between the efficacy of ginger and sumatriptan in the ablative treatment of the common migraine.”