top of page

Anafailaksia

Mwandishi:

ULY CLINIC

21 Julai 2021 19:12:31

Anafailaksia

Anafailaksia ni nini?


Anafilaksia ni mzio mkubwa wa dawa unaotokea dakika chache tu baada ya kutumia dawa au kitu kinachosababisha mzio. Hali hii inahitaji matibabu ya haraka sana ilikuokoa maisha ya muathirika.

Dalili


Dalili za anafailaksia ni;


 • Kupoteza fahamu

 • Kuvimba kwa ngozi, kutokwa jasho au kupauka au kupasuka na kutokwa na malengelenge makubwa

 • Kuhisi joto la ghafla baada ya kutumia dawa

 • Kuhisi unakabwa na kitu shingoni

 • Kichefuchefu, kutapika au kuharisha

 • Maumivu ya tumbo

 • Mapigo ya moyo kwenda haraka

 • Mapigo ya mishipa ya damu kwenda haraka

 • Kutokwa na kamasi

 • Kupiga chafya

 • Kuvimba kwa ulimi na midomo

Imeboreshwa,

6 Juni 2022 15:00:43

bottom of page