top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

14 Juni 2021, 20:51:57

Antibodi

Antibodi

Antibodi ni nini?


Antibodi ni ni protini zinazozalishwa kwenye damu kuitikia uwepo wa antijeni kwenye damu.


Antibodi huungana kikemia na antijeni na matokeo yake ni kuuliwa/ kuharibiwa kwa antijeni. Seli za limfu B huzalishwa kwa mara ya kwanza ili kushambulia vimelea walioingia mwilini, baada ya shambulio kutokea, seli za limfu B huamsha uzalishaji wa antibodi ambazo zitaishi kwenye damu tayari kwa kupambana na vimelea kama huyo atakapoingia kwenye mwili kwa mara nyingine.


Namna ya kutamka antibodi


Neno antibodi hutamkwa kama 'antibadi'

Imeboreshwa,

21 Mei 2025, 08:44:19

bottom of page