top of page

Kukosa uwezo wa spasho

Mwandishi:

ULY CLINIC

23 Julai 2021 20:58:38

Kukosa uwezo wa spasho

Kukosa ujuzi wa spasho maaana yake nini?


Kukosa ujuzi wa spasho ni kukosekana kwa uwezo wa mtu kuchakatua kile anachokiona ili kuelewa uhusiano wake na vitu vingine pamoja na kuangalia madhari au picha tofauti. Uwezo wa kispasho ni uwezo wa mtu kuona na kuelewa uhusiano wa vitu na kutumia uhusiano huo kutengeneza au kubadilisha vitu vilivyoona.


Maswali ambayo yanaweza kushuku upotevu wa uwezo wa kispasho ni;


  • Je mtoto wako anachanganya kushoto na kulia?

  • Je mtoto anapata shida kuchora kunukuu maandishikutoka kwenye kitabu au ubao

  • Je mtoto anashindwa kupanga vitu kwenye loka au kwenye chumba chake au meza?

  • Je mtoto anapotea kirahisi haswa kwenye mazingira mapya?

  • Je mtoto anashindwa kuelewa ramani?

  • Je mtoto anagongana na watu kurahisi au kushindwa kukadilia umbali kati yake na wengine?

  • Je mtoto anashindwa kuumba maumbo licha ya kuwa na mfano wa picha?

Imeboreshwa,

6 Juni 2022 14:51:46

bottom of page