Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
21 Julai 2026, 05:35:43

UTI
UTI hutumiwa na watu wengi kumaanisha U.T.I ambacho ni kifupi cha neno Urinary Tract Infection,kwa kiswahili hufahamika kama maambukizi kwenye njia ya mkojo na kitiba humaanisha maambukizi kwenye mfumo wa mkojo.
Hivyo UTI, U.T.I au uti, u.t.i ni maambukizi ya vimelea katika mfumo wa mkojo yanayopelekea kuonekana kwa dalili mbalimbali kama vile maumivu wakati wa kukojoa, hisia za kuungua wakati wa kukojoa na kukojoa mara kwa mara. Mara nyingi UTI husababishwa na bakteria, marachache vimelea wengine kama virusi na fangasi wanaweza kusababisha ugonjwa huu.
UTIÂ ni kifupi cha maneno ya Kiingereza Urinary Tract Infection, ambayo kwa Kiswahili huitwa maambukizi kwenye mfumo wa mkojo.
UTI ni maambukizi yanayosababishwa na kuingia na kuongezeka kwa vijidudu kwenye sehemu yoyote ya mfumo wa mkojo, unaojumuisha figo, mirija ya yureta, kibofu cha mkojo na mrija ya kutoa mkojo nje ya kibofu (yurethra). Mara nyingi husababishwa na bakteria, hasa Escherichia coli (E. coli), ingawa fangasi na virusi vinaweza kusababisha UTI katika hali maalumu.
Dalili za kawaida ni maumivu au kuungua wakati wa kukojoa, kukojoa mara kwa mara, kuhisi kubanwa na mkojo, maumivu chini ya kitovu na wakati mwingine damu kwenye mkojo. UTI hugunduliwa kwa vipimo vya mkojo na kutibiwa kulingana na chanzo chake, mara nyingi kwa dawa za antibiotiki.
Tazama pia:Â Sistaitisi, Payelonefraitisi, Yurethraitisi, Yurinalisisi, Kuotesha mkojo, Bakteria kwenye mkojo(Bakteriyuria).
Imeandikwa:
31 Mei 2022, 15:53:02
