Imeandikwa na mdaktariwa ULY-Clinic
Kukosa usingizi- Insomnia
Utangulizi
Insomnia ni neno tiba lililotokana na neno la kiratini in- kukosa na somnus- usingizi, neno tiba hili lili anza kutumika kwenye matibabu likimaanisha kukosa usingizi katika karne ya 17
Kukosa usingizi (insomnia) ni tatizo endelevu linalosababisha mtu kushindwa kuanza kusinzia, kutodumu kwenye usingizi ama vyote viwili licha ya kupata fursa ya kulala ipasavyo. Kwa kukosa usingizi, mtu huyu kwa kawaida huamka hajihisi kuwa mpya , hali hii inasababisha kupunguza uwezo wa kufanya kazi wakati wa mchana.kukosa usingizi hakumalizi nguvu tu na hali yako, bali hudhuru afya na ubora wa maisha.
Usingizi kiasi gani unatosha hutegemea mtu moja na mwingine,mara nyingi watu wazima huhitaji masaa 7 hadi nane ya kulala.
Watu wengi pia walishawahi au watapata tatizo la kukosa usingizi kipindi Fulani katika maisha yao lakini huwa si endelevu lakini baadhi wanaweza kupata tatizo hili na kuwa endelevu. Kukosa usingizi kupo kwa aina mbili yaani aina ya kwanza na aina ya pili amabayo husababishwa na madawa au ugonjwa mwilini.
Huhitaji kutolala usiku, mabadiliko ya mambo Fulani katika maisha yako yanaweza kukusaidia kupata usigizi.
ULY clinic inakukumbusha uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ya kiafya.