top of page

Mwandishi:

WAMJW

Mhariri:

ULY CLINIC

9 Oktoba 2021, 09:59:57

Barakoa baada ya chanjo

Je, mtu akichanjwa chanjo ya Corona anatakiwa aendelee kuvaa barakoa?

NDIO!

Nini inashauri kuwa mtu aendelee kujikinga hata baada ya kupata chanjo ya COVID-19 kwa sababu zilizoorodheshwa kwenye aya zinazofuata.


Lengo kubwa na la msingi la Chanjo ya COVID-19 siyo kukukinga usipate maambukizi, ila Lengo na Faida kubwa na zenye kulengwa kwenye ya chanjo za COVID-19 ni kuzuia mtu asipate ugonjwa mkali na pia kumkinga asife endapo atapata ugonjwa wa COVID-19. Hivyo, ingawa chanjo inaweza kukukinga kwa kiasi fulani usipate maambukizi lakini bado baada ya kupata chanjo unaweza kupata maambukizi na kuambukiza wengine pia – hivyo kuna umuhimu wa kuendea kujikinga


Baada ya kupata chanjo, kinga mwilini ujijenga kidogo kidogo mpaka wiki ya pili hadi mwezi mmoja baada ya dozi ya mwisho ya chanjo.


Hivyo, kwa kipindi hicho mwili unapoendelea kujijengea kinga, mtu anaweza kupata maambukizi na kuugua na hata kupoteza maisha kwani mwili bado unakuwa haujawa na kinga ya kutosha kukulinga kikamilifu, hivyo basi kuna umuhimu wa kuendelea kujikinga mpaka mwili ujenge kinga ya kutosha.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

9 Oktoba 2021, 12:28:12

Rejea za mada hii

bottom of page