top of page

Mwandishi:

WAMJW

Mhariri:

ULY CLINIC

9 Oktoba 2021, 09:56:03

Chanjo ya COVID-19 inatolewa kwa watu gani?

Chanjo ya COVID-19 inatolewa kwa watu gani?

Chanjo za COVID-19 ni salama kwa watu wengi wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea, ikiwa ni pamoja na wale wenye magonjwa sugu kama vile: Shinikizo la damu, ugonjwa wa kisukari, pumu, na magonjwa mengine mfumo wa hewa, magonjwa ya ini na figo. Pia chanjo ni salama kwa wale wanaoishi na virusi vya UKIMWI, lakini siyo kwa wale waliozidiwa.


Kwa awamu ya kwanza, Tanzania iliingiza nchini dozi za kutosha takribani watu milioni moja, hivyo Serikali iliona ni busara kuwapa kipaumbele makundi yafuatayo;


  1. Wataalam wa Afya

  2. Watu wenye umri wa miaka 50 na kuendelea na

  3. Wale wenye magonjwa sugu.


Lakini kuanzia Agosti 12, 2021 Serikali iliruhusu chanjo za COVID-19 zitolewe kwa mtu yeyote mwenye miaka 18 na kuendelea atakayekuwa anahitaji chanjo kwa hiari yake.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

9 Oktoba 2021, 12:28:12

Rejea za mada hii

bottom of page