top of page

Mwandishi:

WAMJW

Mhariri:

ULY CLINIC

9 Oktoba 2021 10:23:24

Chanjo ya COVID-19 ni ya kudumu?

Mtu akipata chanjo ya COVID-19 anakuwa amepata kinga ya kudumu dhidi ya COVID-19?

Mpaka sasa tafiti zinaendelea kufanyika ili kuchunguza kama mtu akipatiwa chanjo ya COVID-19 anakuwa amepata kinga ya kudumu au anatakiwa kuchoma dozi nyingine baada ya kipindi fulani. Na kama anavyojua hiki kirusi cha Corona kimekuwa kikibadilika badilika kila baada ya muda na hatujui haya mabadiliko yakiendelea yataathiri ufanisi wa chanjo zilizopo kwa kiwango gani, na ndio maana bado tafiti zinaendelea kufanya sehemu mbalimbali duniani ili kutafuata majibu ya haya maswali. Hata hivyo,

chanjo za COVID-19 zinazuia mtu kupata ugonjwa mkali, kulazwa au kifo hata anapoambukizwa na anuai

mpya za virusi vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

9 Oktoba 2021 12:28:08

Rejea za mada hii

bottom of page