top of page

Mwandishi:

WAMJW

Mhariri:

ULY CLINIC

9 Oktoba 2021 10:18:01

Chanjo ya COVID ni mpango wa kupunguza watu duniani?

Je, chanjo ni njia inayotumiwa na mataifa makubwa kupunguza idadi ya watu duniani? Na je Corona ilitengenezwa kwa ajili ya kupunguza watu duniani?

Hakuna ushahidi!

Lengo kubwa la chanjo, ikiwa ni pamoja na hizi chanjo za COVID-19 ni kumkinga mtu aliepatiwa chanjo ama asipate maambukizi au asipate madhara makubwa au kumkinga na kifo kitokanacho na ugonjwa husika.


Ndio maana faida kubwa ya chanjo ya COVID-19 ni kumkinga mtu asipate COVID-19 kali au kumkinga na kifo kitokanacho na COVID-19. Hivyo basi hakuna ushahidi wowote wa kisayansi wa chanjo zilizopo ikiwa ni pamoja na chanjo ya COVID-19 kuathiri kwa namna yoyote ile mfumo wa via vya uzazi au kupunguza idadi ya watu. Na ndio maana tangu utotoni tumekuwa tumepata chanjo mbalimbali ikiwa ni pamoja na chanjo za Kifua kikuu, polio, surua, pepopunda na kadhalika, lakini hazijawahi kuathiri uweze wa watu kuzaa. Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) ilichunguza chanjo hizi na kujiridhisha pasipo shaka kuwa hakuna kitu chochote ndani ya chanjo kinachoweza kuathiri mfumo wa uzazi.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

9 Oktoba 2021 15:24:13

Rejea za mada hii

bottom of page