Mwandishi:
WAMJW
Mhariri:
Dkt. Benjamin L, MD
9 Oktoba 2021 06:11:48
Je, anuai ya Delta ya virusi vinavyosababisha COVID-19 ilitokea vipi?
Anuai mpya ya Delta imetokana na mabadiliko ndani ya vinasaba vya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19. Mabadiliko haya yamepelekea kirusi hiki;
Kuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kuambukiza
Kusambaa na kusababisha ugonjwa mkali wa UVIKO-19
Mabadiliko katika vinasaba vya virusi vinavyosababisha UVIKO-19 hutokea kwa urahisi mara pindi virusi hivi vinapokuwa ndani ya watu wenye upungufu wa kinga mwilini hali ambayo inaruhusu mabadiliko hayo kwa urahisi zaidi
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
9 Oktoba 2021 09:50:39
Rejea za mada hii
https://www.who.int/emergencies/diseases/novel-coronavirus-2019/question-and-answers-hub. Imechukuliwa 09.10/2021