Mwandishi:
Dkt. Adolf S, M.D
Mhariri:
Dkt. Sospeter B, MD
22 Julai 2023, 18:48:14

Fluconazole inatibu nini?
Fluconazole ni mojawapo ya dawa zilizo katika kundi la dawa za kutibu fangasi. Dawa hii hutumika kutibu magonjwa mbali mbali yanasobabishwa na fangasi kama vile;
Fangasi wa ukeni
Fangasi wa mdomoni
Fangasi wa koo la chakula
Fangasi wa ngozi
UTI inayosababishwa na fangasi
Peritonaitis inayosababishwa na fangasi
Homa ya uti wa mgogo inayosababishwa na fangasi
Nimonia inayosababishwa na fangasi
Maambukizi ya fangasi katika damu
Kumbuka
Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu FLuconazole kwenye makala ya Fluconazole
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
22 Julai 2023, 18:48:14
Rejea za mada hii
Fluconazole – StatPearls – NCBI Bookshelf. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK537158/. Imechukuliwa 22.07.2023.
Antifungal Drugs – Infectious Diseases – MSD Manual Professional Edition. https://www.msdmanuals.com/professional/infectious-diseases/fungi/antifungal-drugs. Imechukuliwa 22.07.2023.
Oral therapy of common superficial fungal infections of the skin – PubMed. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/10367914/. Imechukuliwa 22.07.2023.