top of page

Mwandishi:

Dkt Benjamin L, MD

Mhariri:

Dkt. Mangwella S, MD

14 Novemba 2021 19:48:29

Je, kuna madhara ya hepatitis B kwa mjamzito?

Je, kuna madhara ya hepatitis B kwa mjamzito?

Hepatitis B ni ugonjwa wa ini unaotokana na maambukizi ya kirusi hepatitis B. mama mjamzito mwenye maambukizi ya kirusi hiki anaweza kumwambukiza mtoto tumboni.


Je, hatari ya mtoto kupatamaambukizi ni katika kipindi gani cha ujauzito?


Wakati hatari ya mtoto tumboni kupata Hepatiti B inatofautiana katika vipindi vitatu vya ujauzito, mtoto ana hatari kubwa ya kupata maambukizi kwenye kipindi cha tatu cha ujauzito.


Je, ni madhara gani ya hepatitis B kwa mtoto aliyepata maambukizi kutoka kwa mama?


Asilimia 90 ya watoto waliopata maambukizi wakati wakiwa tumboni mwa mama au wakati wa kujfungua wana hatari ya kuugua ugonjwa sugu wa hepatitis B na takribani asilimia 25 ya watoto wenye ugonjwa sugu wa hepatis B katika mwaka wa kwanza, hupata ugonjwa sugu wa ini. Madhara mengine ni kupata saratani ya ini hapo baaadae.


Unawezaje kuzuia madhara kwa mtoto?


Unaweza kuzuai mwanao mtarajiwa kupata maambukizi ya Hepatitis B kwa kufanya vipimo kabla ya kubeba mimba au kufanya uchunguzi kabla ya kujifungua na kupatiwa matibabu ya hepatitis B ili kuzuia kichanga kupata maambukizi wakati wa kujifungua.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

14 Novemba 2021 19:48:29

Rejea za mada hii

  1. CDC. Hepatitis B in pregnancy. https://www.cdc.gov/hepatitis/HBV/PerinatalXmtn.htm. Imechukuliwa 14.1.2021

  2. Sookoian S. Liver disease during pregnancy: acute viral hepatitis. Ann Hepatol 2006; 5:231.

  3. Stevens CE, et al. Perinatal hepatitis B virus transmission in the United States. Prevention by passive-active immunization. JAMA 1985; 253:1740.

bottom of page