top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

ULY CLINIC

1 Septemba 2023 17:18:43

Je, kwenye dirisha la matazamio unaweza kuambukiza VVU?

Je, kwenye dirisha la matazamio unaweza kuambukiza VVU?

Ndio, unaweza kumwambukiza mtu mwingine VVU ukiwa kwenye dirisha la matazamio haswa endapo upo kwenye kihatarishi kikubwa. Inafahamika kuwa, kwenye dirisha la matazamio, mtu anakuwa kwenye hatari kubwa ya kuambukiza wengine licha ya kutogundulika kuwa na maambukizi kwa kipimo.


Dirisha la matazamio ni muda kati ya siku ya kupata maambukizi mpaka kutambulika kwa kipimo cha damu. Muda huu hutotegemea aina ya kipimo, kuna baadhi ya kipimo hutambua maambukizi mapema zaidi kuliko kawaida.


Je, nini huongeza hatari ya ya kuambukiza wengine

Hatari kubwa ya kumwambukiza mwingine wakati upo kwenye dirisha la matazamio hutegemea aina ya kihatarishi cha maambukizi;


Kutumia dawa za kulevya kwa kuchangia sindano

Kati ya watu 100,000 unaweza kuambukiza watu 49.


Kujihusisha na mapenzi ya mwanaume kwa mwanaume

Kati ya watu 100,000/= unaweza kuambukiza watu 42.


Kuuza ngono

Kati ya watu 100,000, unaweza kuambukiza watu 27.


Kushiriki ngono ya hatari

Kati ya watu 100,000 unaweza kuambukiza watu 3.


Nini cha kufanya ili usiambukize wengine

Endapo unahisi upo kweye hatari ya kupata maambukizi kwa kujihusisha na kihatarishi chochote, unapaswa kutumia kinga kujilinda na kuwalinda wengine kupata maambukizi ya VVU.


Jifunze zaidi kuhusu maambukizi PEP na PrEP katika kuzuia maambukizi ya UKIMWI kabla au baada ya kujihatarisha katika makala huzika.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

1 Septemba 2023 17:33:12

Rejea za mada hii

  1. Kucirka LM, Sarathy H, Govindan P, Wolf JH, Ellison TA, Hart LJ, Montgomery RA, Ros RL, Segev DL. Risk of window period HIV infection in high infectious risk donors: systematic review and meta-analysis. Am J Transplant. 2011 Jun;11(6):1176-87. doi: 10.1111/j.1600-6143.2010.03329.x. Epub 2011 Mar 2. PMID: 21366859; PMCID: PMC3110509.

  2. HIV. Https://i-base.info/guides/testing/what-is-the-window-period#:Imechukuliwa 01.09.2023.

  3. What is the window period for an HIV test?. Window period. https://www.cdc.gov/hiv/basics/hiv-testing/hiv-window-period.html. Imechukuliwa 01.09.2023.

bottom of page