Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD
Mhariri:
Dkt. Sospeter M, MD
20 Novemba 2021, 17:37:50
Je, ni nani anaweza kutumia majira yenye vichocheo viwili?
Wanawake wenye watoto au wasio na watoto, ambao hawajaolewa, wenye VVU, walio chini ya miaka 35 na wanavuta sigara, waliotoa mimba au kuharibikiwa mimba wanawezakutumia vidonge hivi.
Majira yenye vichocheo viwili inaweza kutumika kwa wanawake wenye sifa zifuatazo;
Wenye watoto au hawajawahi kuwa nao
Ambao hawajaolewa
Wa umri wowote, pamoja na vijana na wanawake wenye umri zaidi ya miaka 40
Ambao wametoa mimba au mimba imeharibika
Wanaovuta sigara kama wana umri chini ya miaka 35
Wana upungufu wa damu sasa au walikuwa nayo siku za nyuma
Wana vena varikosi
Wenye maambukizi ya VVU, kama wameanza au hawajaanza kutumia dawa za kupunguza makali ya UKIMWI (Soma zaidi kuhusu majira yenye vichocheo viwili kwa Wanawake wenye VVU)
Soma zaidi kuhusu majira yenye vichocheo viwili kwenye makala za uzazi wa mpango.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
20 Novemba 2021, 17:54:21
Rejea za mada hii
Who Can and Cannot Use Combined Oral Contraceptives. https://www.fphandbook.org/who-can-and-cannot-use-combined-oral-contraceptives. Imechukuliwa 20.11.2021
Baird DT, et al. Hormonal contraception. N Engl J Med. 1993 May 27;328(21):1543-9.
Maguire K, et al. The state of hormonal contraception today: established and emerging noncontraceptive health benefits. Am J Obstet Gynecol. 2011 Oct;205(4 Suppl):S4-8.
Committee on Gynecologic Practice. ACOG Committee Opinion Number 540: Risk of venous thromboembolism among users of drospirenone-containing oral contraceptive pills. Obstet Gynecol. 2012 Nov;120(5):1239-42.
Shulman LP. The state of hormonal contraception today: benefits and risks of hormonal contraceptives: combined estrogen and progestin contraceptives. Am J Obstet Gynecol. 2011 Oct;205(4 Suppl):S9-13. [PubMed]
ACOG Practice Bulletin No. 110: noncontraceptive uses of hormonal contraceptives. Obstet Gynecol. 2010 Jan;115(1):206-218.
Simmons KB, et al. Drug interactions between non-rifamycin antibiotics and hormonal contraception: a systematic review. Am J Obstet Gynecol. 2018 Jan;218(1):88-97.e14.
Weerasinghe M, et al. Overdose of oral contraceptive pills as a means of intentional self-poisoning amongst young women in Sri Lanka: considerations for family planning. J Fam Plann Reprod Health Care. 2017 Apr;43(2):147-150.