top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter B, MD

Mhariri:

Dkt. Ben A, MD

28 Mei 2023, 10:53:30

Je, PEP ina ufanisi gani?

Je, PEP ina ufanisi gani wa kuzuia maambukizi ya UKIMWI baada ya kujihatarisha??

Mambo ya kufahamu wakati unasoma makala hii


  • Kunywa PEP ndani ya masaa 72 huwa na ufanisi mkubwa wa kuzuia maambukizi

  • PEP ina ufanisi mkubwa zaidi kama ikitumika mara tu baada ya kihatarishi na kwa muda wa siku 28 bila kukosea dozi

  • Ili uweze kuwa salama, chukua hatua za ziada kujizuia wewe na wengine kupata maambukizi wakati unatumia PEP

  • Hatua hizo zinajumuisha kutumia kondomu, kutoshiriki sindano za madawa ya kulevya na vifa vingine vya kujidunga dawa

  • Wengi wanaopata maambukizi ya VVU licha ya kutumia PEP ni wale wanaoendelea kujiweka kwenye kihatarishi

 

Je PEP ina ufanisi gani wa kukinga na maambukizi ya VVU?

 

Njia sahihi ya kupima ufanisi wa PEP ni kwa kufanya tafiti ya makundi mawili ya watu wanaotumia PEP baada ya kujihatarisha na wale wasiotumia PEP. Hata hivyo tafiti hiii haiwezi kufanyika kwa kuwa ni tofauti na maadili kutompatia dawa mtu aliye kwenye hatari ya maambukizi kwa nia ya kufahamu kama atapata maambukizi au la.


Njia pekee inayotumika kwa sasa ni kuangalia wanaotumia dawa baada ya kuwa kwenye kihatarishi ambapo tafiti mbalimbali zimeanyika na kuonyesha kuwa PEP ina ufanisi mkubwa.

 

Mwaka 2016, CDC marekani walifanya tafiti sita za kuangalia watu wanaotumia PEP na matokeo ya baadhi ya tafiti ni kama yanavyoonekana hapa chini:

 

Tafiti ya kwanza

 

Inatokana na muunganiko wa tafiti 6 ambazo zilifuatilia wanaume 1535 waliokuwa wanatumia PEP baada ya kihatarishi.

 

Kati ya wanaume hao 1535 , wanaume 1487 hawakupata maambukizi wakati wanaume 48 walipata maambukizi. Kati ya hao 48 waliopata maambukizi:

  • 40 sababu ilielezewa kuwa ni kuendelea kujihusisha na kihatarishi wakati wanatumia dawa. 35 kati ya 40 maambukizi yalitokea zaidi ya miezi 6 baada ya kuanza PEP ambapo ni dhahiri kuwa si kwa sababu ya kushindwa kufanya kazi kwa PEP

  • 8 waliobaki ni kwa sababu ya kufeli kufanya kazi kwa dawa, hii ni sawa na asilimia 0.5% ya watumiaji.

 

Tafiti ya 2

 

Inatokana na muunganiko wa tafiti 15 ambazo ziliwafutilia jumla ya watu  2209 waliojumuisha watoto, vijana wadogo, na watu wazima ambao walijihusisha na vitendo vya ngono ya kukubaliana, kubakwa, kujidunda dawa za kulevya kwa kushiriki sindano na ajali ya kujichoma sindano.

 

Kati ya watu 2209, watu 2190 hawakupata maambukizi wakati watu 19 walipata maambukizi

Kati ya waliopata maambukizi, watu 18 ilikuwa kwa sababu ya kutozingatia dozi ya dawa na kuendelea kujiweka kwenye kihatarishi na mmoja aliyebaki ilionekana ni kutokana na kushindwa kufanya kazi kwa dawa.

 

Nini cha kujifunza kwenye tafiti hii?

 

Kwa ujumla kutokana na tafiti hiyo imeonyesha kuwa watu wanaopata maambukizi licha ya kutumia PEP ni wale ambao:

  • Hawajanza PEP kwa wakati

  • Hawajatumia dawa kwa usahihi ( kukosa dozi au kutotumia kwa siku 28 mfululizo)

  • Kuwa na kirusi mwenye usugu kwenye dawa

  • Kutumia dawa zenye uwezo mdogo wa kupenya kwenye via vya ngono(Dawa hizo hazishauriwi kutumika kwa sasa)

  • Kujihusisha na ngono isiyo salama au kuendelea kuwa kwenye kihatarishi wakati unatumia PEP


Majibu ya makala hii

Maswali yanayojibiwa na makala hii

  • Je PEP ina ufanisi gani wa kuzuia maambukizi ya VVU?

  • Je ninaweza kuzuia kupata maambukizi ya UKIMWI nikitumia PEP

  • Je nawezaje kuongeza ufanisi wa dawa za PEP?

  • Je wakati natumia PEP naruhusiwa kushiriki ngono bila kinga?

  • Je nawezaje kumzuia mpenzi wangu kupata maambukizi wakati natumia PEP

  • Je nikikosa dozi ya PEP naweza kupata maambukizi?

  • Je dawa za PEP zinatumika kwa muda gani?

  • Je kua uhaja wa kutumia dawa za PEP kwa siku 28?


Maelezo zaidi kuhusu PEP

Wapi unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu PEP

Kwa maelezo zaidi kuhusu PEP soma makala ya PEP au dawa za kukinga UKIMWI ndani ya masaa 72


Je vipi kuhusu PrEP?

Kufahamu kuhusu PrEP ingia kwneye makala ya PrEP au video ya PrEP

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

28 Mei 2023, 10:53:30

Rejea za mada hii

bottom of page