top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

ULY CLINIC

12 Agosti 2023 17:44:45

Je, unatumbua vipi kama una PID?

Je, kuna kipimo maalumu cha PID

Hakuna kipimo cha utambua kama una PID. Utambuzi wa sasa mara nyingi hutokana na historia ya kitabibu inayochukuliwa kwako sambamba na uchunguzi wa awali wa mwili pamoja na vipimo vingine. Mara nyingi unaweza usitambue kuwa una PID kwa sababu dalili huwa za wastani au kutotokea kabisa. Hata hivyo endapo zitatokea hujumuisha;


 • Maumivu kwenye tumbo la chini ya kitovu

 • Homa

 • Kutokwana uchafu wenye harufu mbaya ukeni

 • Hisia za kuungua wakati wa ngono

 • Kutokwa na damu ukeni wakati wa ngono

 • Pain in your lower abdomen;

 • Hisia za kuungua wakati w akukojoa

 • Kutokwa na damu katikati ya vipindi vya hedhi


Mambo ya kukumbuka

Mbali na dalili hizi kuashiria PID, unapaswa kupata uchunguzi wa daktari ili aweze kutambua kama ni PID au ugonjwa mwingine na kupata matibabu sahihi.


Wapi unaweza kupata maelezo zaidi?

Pata maelezo zaidi katika makal aya PID sehemu nyingine katika makala zifuatazo

 • Je PID inatibika

 • Ugonjwa wa PID

 • Majadiliano na wataalamu wa afya PID


ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

12 Agosti 2023 17:44:45

Rejea za mada hii

 1. American College of Obstetricians and Gynecologists (ACOG). Pelvic Inflammatory Disease. ACOG Patient Education Pamphlet, 1999.

 2. Westrom L and Eschenbach D. In: K. Holmes, P. Sparling, P. Mardh et al (eds). Sexually Transmitted Diseases, 3rd Edition. New York: McGraw-Hill, 1999, 783-809.

bottom of page