top of page

Mwandishi:

Dkt. Mangwella S, MD

Mhariri:

Dkt. Charles W, MD

17 Oktoba 2021 16:05:16

Je maziwa ya ngombe husababisha upungufu wa damu kwa watoto?

Je maziwa ya ngombe husababisha upungufu wa damu kwa watoto chini ya umri wa mwaka mmoja?

Ndio!

Kuwapa maziwa ya ng’ombe watoto walio chini ya umri wa mwaka mmoja huathiri kiwango cha madini chuma mwilini kiasi cha kupelekea kupta upungufu wa damu.


Kwanini upungufu huu hutokea?


Kuna njia mbalimbali za kisayansi zinazoelezea kwanini upungufu wa madini chuma na damu unaweza kutokea, amabzo ni;


 • Kuna kiasi kidogo cha madini chuma kwenye maziwa ya ng’ombe, kiasi cha kushindwa kutosheleza mahitaji ya mwili kutengeneza damu na ukuaji.

 • Maziwa ya ng’ombe huongeza upotevu wa damu kwenye kinyesi kwenye asilimia 40 ya watoto wenye afya njema

 • Kuna kiasi kikubwa cha casein na kalisiamu kweye maziwa ya ng’ombe kinachozuia ufyonzwaji wa madini chuma yasiyo na asili ya heme. Takribani asilimia 10 tu ya madini chuma kwenye maziwa ya ng’ombee hufyonzwa na kuingia mwilini.


Je mtoto anaweza kutumia maziwa ya ng’ombe baada ya kuvuka mwaka mmoja?


Ndio!

Upotevu wa madini chuma kwenye kinyesi hupungua jinsi mtoto anavyoongezeka umri na husimama baada ya kuvuka umri wa mwaka mmoja.


Je kuna njia za kuandaa maziwa ya ngombe kudhibiti upungufu wa madini chuma kwa mtoto?


Baadhi ya nchi huongeza virutubishi na madini kwenye maziwa ya ngombe baada ya kuchemshwa kwenye joto kali ili kuua vimelea na kuondoa baadhi ya protini. Maziwa yaliyotengenezwa namna hii huweza kutumika kwa watoto kudhibiti upungufu wa madini chuma kama mbadala wa maziwa ya ngombe tupu. Hata hivyo inashauriwa matumizi ya maziwa yawe ya wastani tu.


Mambo mengine unayotakiwa fahamu kuhusu maziwa ya ng’ombe kwa mtoto


 • Maziwa ya ng’ombe huwa na chumvi nyingi kuliko maziwa ya mama

 • Huwa na protini kwa wingi inayoweza kuongeza hatari ya uzito mkubwa na obeziti kwa mtoto


Soma zaidi kuhusu maziwa ya ng'ombe kwa mtoto kwa kubofya hapa.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

17 Oktoba 2021 16:53:06

Rejea za mada hii

 1. Ziegler EE, et al. Cow milk feeding in infancy: Further observations on blood loss from the gastrointestinal tract. J Pediatr. 1990;116:11–8

 2. Wilson JF, Lahey ME, Heiner DC. Studies on iron metabolism. V. Further observations on cow’s milk-induced gastrointestinal bleeding in infants with iron-deficiency anemia. J Pediatr. 1974;84:335–44.

 3. Bu, Guanhao et al. “Milk processing as a tool to reduce cow's milk allergenicity: a mini-review.” Dairy science & technology vol. 93,3 (2013): 211-223. doi:10.1007/s13594-013-0113-x

 4. Leung AK, Chan KW.Iron deficiency anemia Adv Pediatr(In press)

 5. Tunnessen WW, et al. Consequences of starting whole cow’s milk at 6 months of age. J Pediatr. 1987;111:813–6.

 6. Penrod JC, et al. Impact of iron status of introducing cow’s milk in the second six months of life. J Pediatr Gastroenterol Nutr. 1990;10:462–7.

 7. de Andraca I, et al. Psychomotor development and behavior in iron-deficiency anemic infants. Nutr Rev. 1997;55:125–32.

 8. Ziegler EE. Consumption of cow's milk as a cause of iron deficiency in infants and toddlers. Nutr Rev. 2011 Nov;69 Suppl 1:S37-42. doi: 10.1111/j.1753-4887.2011.00431.x. PMID: 22043881.

bottom of page