top of page

Mwandishi:

WAMJW

Mhariri:

Dkt. Mangwella S, MD

10 Oktoba 2021 12:10:53

Je mtu aliyeugua COVID-19 zaidi ya mara moja ana kinga zaidi ya kutohitaji chanjo?

Je tafiti zinasemaje kuhusu mtu aliyeugua akapona akaugua tena, je, kuna kuwa na utofauti na mtu aliyechanjwa? Nani anakuwa na unafuu?

Tafiti zimeonyesha kwamba mtu aliyeugua anapata kinga ya muda na ana uwezekano wa kupata maambukizi mapya. Chanjo husababisha mwili kutengeneza kinga nyingi zaidi kuliko kinga inazotengenezwa na mwili kutokana na maambukizi ya virusi vinavyosababisha COVID-19. Virusi vya COVID-19 hujificha viwapo mwilini na kusababisha mfumo wa kinga kutokuvitambua vyema hali inayosababisha mwili kutotengeneza kinga za kutosha. Hivyo, ni muhimu mtu aliyeugua kawaida kuchanjwa baada ya kupona.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

10 Oktoba 2021 12:11:01

Rejea za mada hii

bottom of page