Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Benjamin L, MD
23 Oktoba 2021 07:30:54
Kutoboka kwa meno husambaa kati ya jino moja na jingine?
Utando wa bakteria unaotokana na kunywa na kula vitu vitamu pamoja na kutofanya usafi wa meno husababishi kutoboka na kuoza kwa jino. Jino lililooza haliwezi kuambukiza jino jirani, jino jirani huoza kama kuna visababishi tu.
Visababishi vya kutoboka na kuoza kwa meno
Kuoza au kutoboka kwa meno mara zote husababishwa na muunganiko wa mambo matatu yaliyoelezewa hapa chini;
Utando wa bakteria kufunika jino ambao umetengenezwa kwa bakteria mabaki ya chakula na mate kwa mtu anayekula au kunywa vyakula vyenye sukari na kutofanya vema usafi wa kinywa. Bakteria wanaovunja ukuta huu pamoja na sukari iliyopo kwenye ukuta husababisha kutengenezwa kwa tindikali kwenye ukuta wa jino. Kama jino lisiposafishwa kila siku, tindikali hula ukuta wa jino taratibu na kuufanya uwe dhaifu na kutoboka au kuoza.
Jino zima linaweza kupata maambukizi kwenye jino lililooza?
Hapana
Jino lililooza haliwezi kuambukiza jino ambalo halijaoza. Jino jirani na jino lililooza linaweza kuoza au kutoboka endapo lina visababishi vitatu vilivyotajwa hapo juu.
Licha ya meno kuoza kutosambaa kati ya jino moja na jingine, bakteria wanaosababisha meno kuoza wanaweza kusambaa kati ya jino moja na jingine.
Wapi unaweza pata maelezo zaidi?
Jifunze zaidi kuhusu meno kuoza na kutoboka au namna ya kujikinga na meno kutoboka ndani ya mada za ULY CLINIC
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
23 Oktoba 2021 07:35:36
Rejea za mada hii
NCBI. Tooth decay: Overview. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK279514/. Imechukuliwa 23.10.2021