Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
ULY CLINIC
29 Mei 2025, 17:40:05

Kwa nini mwanamke anaweza kushindwakufika kileleni? Fahamu sababu na namna ya kutatuta
Maelezo ya singi
Nimekuwa na shida tangu nilipoanza kushiriki tendo la ndoa. Sijawahi kufika kileleni wakati wa tendo. Kuna siku chache ambazo nimesikia hali fulani ya raha mwilini, ambayo nahisi ndio kilele, lakini hii hujitokeza muda mfupi baada ya mwenza wangu kumaliza tendo, si wakati wa tendo lenyewe. Katika mara kumi tofauti nilizofanya tendo, hali hiyo ya kufika kileleni imetokea mara mbili pekee. Nimekuwa nikijiuliza kwa nini siwezi kufika kileleni mara kwa mara kama wengine na kama kuna dawa salama zinazoweza kusaidia.
Majibu
Kufika kileleni ni nini?
Kufika kileleni ni kilele cha raha ya ngono ambapo misuli ya uke na eneo la nyonga hukaza kwa kurudiarudia, sambamba na hisia ya kuridhika na utulivu wa mwili na akili. Kwa wanawake, kufika kileleni ni hali ya kipekee na hutofautiana kati ya mtu na mtu, kwa baadhi hufikiwa kwa haraka, kwa wengine huchelewa au kutofika kabisa.
Sababu zinazoweza kuzuia kufika kileleni
1. Sababu za kisaikolojia
Msongo wa mawazo, wasiwasi, au hofu ya kushindwa kufika kileleni
Kukosa kujiamini au hisia hasi kuhusu mwili wako
Kukosa ukaribu wa kihisia na mwenza
2. Sababu za kimwili
Ukosefu wa msisimko wa kutosha kwenye kinembe
Maumivu wakati wa tendo au uke kuwa mkavu
Matatizo ya homoni, kisukari, matatizo ya neva
Madhara ya dawa kama za presha au msongo wa mawazo
3. Sababu za mahusiano na mbinu za tendo
Kukosa maandalizi ya kutosha kabla ya tendo
Kutokuwasiliana na mwenza kuhusu maeneo yako nyeti
Kukosa kushirikiana katika kupeana raha
Je, kuna dawa za kufika kileleni kwa wanawake?
Ndiyo, kuna dawa na virutubisho vinavyolenga kusaidia wanawake kufikia kileleni, lakini ni muhimu kutumia kwa tahadhari na chini ya ushauri wa daktari. Zifuatazo ni baadhi ya dawa:
1. Flibanserin (Addyi®)
Husaidia wanawake wenye kupungukiwa na hamu ya ngono
Hutumika kila siku, lakini hupatikana zaidi marekani na nchi chache sana afrika
Si tiba ya moja kwa moja ya kufika kileleni, ila huongeza hamu
2. Bremelanotide (Vyleesi®)
Sindano inayochochea hisia kabla ya tendo
Haipatikani kwa urahisi Afrika
3. Virutubisho vya asili
Virutubisho hivi vinaweza kupatikana kwenye maduka ya dawa asili au famasi kubwa.
Maca root kutoka kwenye mmea wa kutoka mimea ya Lepidium meyenii– husaidia kuongeza stamina na msisimko
Ginseng – huchochea msisimko wa ngono
Ginkgo biloba – husaidia mzunguko wa damu
L-arginine – huchochea mzunguko wa damu maeneo nyeti
Kumbuka: Virutubisho hivi havipaswi kutumika bila ushauri wa kitaalamu.
Njia salama za kuongeza uwezekano wa kufika kileleni
1. Jitambue Kimwili
Jifunze sehemu zako nyeti, hasa kinembe, na namna zinavyopenda kusisimuliwa
Unaweza kujisaidia kujitambua kwa kujigusa kwa nia ya elimu ya mwili (si kwa lengo la kujichua tu)
2. Kuimarisha misuli sakafu ya nyonga kwa mazoezi
Husaidia kuimarisha misuli ya uke na nyonga
Yanaweza kuboresha msisimko wa ngono na kuleta kufika kileleni ya haraka
3. Kuandaliwa vema na kuwa na mawasiliano
Hakikisha unapata maandalizi ya kutosha kabla ya tendo
Weka wazi kwa mwenza wako kuhusu vitu unavyovipenda kufanyiwa
4. Punguza msongo wa mawazo
Jifunze njia za kupumzika kama yoga au kupumua kwa utaratibu
Kuwa huru kuzungumza na mwenzi wako bila kuhisi aibu
5. Tafuta ushauri wa kitaalamu
Tembelea kliniki ya afya ya uzazi au mshauri wa mahusiano
Wanaweza kusaidia kutambua chanzo cha tatizo na kukupa tiba sahihi
Kumbuka
Wanawake wengi hawafiki kileleni kupitia kuingiziwa uume tu bali kupitia msisimko wa kinembe.
Hali ya kufika kileleni inayochelewa au kutokea baada ya tendo ni ya kawaida, lakini ikiathiri maisha yako ya kimapenzi, ni vyema kutafuta msaada.
Dawa zinaweza kusaidia lakini si mbadala wa mawasiliano, kutambua mwili wako na maandalizi mzuri kabla ya tendo la ndoa.
Hitimisho
Kutofika kileleni si jambo la aibu, na wala halimaanishi kuwa kuna tatizo kubwa – bali ni kiashiria kuwa mwili, akili, au uhusiano unahitaji msaada na uelewa zaidi. Kwa kutumia mbinu sahihi na kuwasiliana kwa uwazi na mwenza, unaweza kubadilisha hali hii na kufurahia tendo la ndoa kwa kuridhika kamili.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
29 Mei 2025, 17:44:08
Rejea za mada hii
American Psychiatric Association. Diagnostic and Statistical Manual of Mental Disorders, Fifth Edition (DSM-5). Arlington, VA: American Psychiatric Publishing; 2013.
Brotto LA, Laan E. Gender and the role of sex hormones in sexual function and dysfunction. J Sex Res. 2015;52(2):1–23. doi:10.1080/00224499.2015.1015713
Kingsberg SA, Woodard T. Female sexual dysfunction: Focus on flibanserin. Clin Obstet Gynecol. 2015;58(4):885–99. doi:10.1097/GRF.0000000000000153
Clayton AH, Kingsberg SA, Goldstein I. Evaluation and management of female sexual dysfunction. J Sex Med. 2018;15(2):184–92. doi:10.1016/j.jsxm.2017.11.022
Meston CM, Hull EM, Levin RJ, Sipski ML. Women’s orgasm. Annu Rev Sex Res. 2004;15(1):173–257.
Althof SE. Psychological and interpersonal dimensions of sexual function and dysfunction. World J Urol. 2011;29(6):659–64. doi:10.1007/s00345-011-0723-3
Hatzimouratidis K, Amar E, Eardley I, Giuliano F, Hatzichristou D, Montorsi F, et al. Guidelines on male sexual dysfunction: Erectile dysfunction and premature ejaculation. Eur Urol. 2010;57(5):804–14. doi:10.1016/j.eururo.2010.01.021
Parish SJ, Goldstein AT, Goldstein SW, Goldstein I, Pfaus JG. Toward a more evidence-based nosology and nomenclature for female sexual dysfunctions – Part I. J Sex Med. 2016;13(12):1888–906. doi:10.1016/j.jsxm.2016.09.019
Krychman ML, Katz A. Sexual health issues in women with chronic medical illnesses. J Sex Med. 2012;9(1):4–9. doi:10.1111/j.1743-6109.2011.02414.x
Leiblum SR. Treating sexual desire disorders: A clinical casebook. New York: Guilford Press; 2007.