Mwandishi:
WAMJW
Mhariri:
ULY CLINIC
9 Oktoba 2021, 09:50:17
Chanjo ya COVID-19 ina madhara gani?
Kama zilivyo dawa, chanjo pia huwa na maudhi madogo madogo. Chanjo dhidi ya COVID-19 kama chanjo wanazopewa Watoto wadogo, nazo pia zina maudhi madogo madogo kama vile;
Homa
Uchovu
Maumivu ya kichwa
Maumivu ya tumbo na maeneo mengine
Maudhi mengineyo
Maudhi haya huisha ndani ya siku 2-3 baada ya kupata chanjo. Iwapo utapata maudhi ambayo hayakutegemewa, unashauriwa kwenda kituo cha afya cha karibu na unapo ishi ili uweze kupata matibabu.
Maudhi makubwa yapo?
Kutokana na mud amfupi tangu kuanza kutumika kwa chanjo za corona, hakuna maudhi makubwa ambayo yameonekana kutokea. Tafiti za hapo mbeleni zitatoa majibu ya swali hili. Hata hivyo baadhi ya maudhi makubwa yanayoweza kutokea kwa watu wachache sana ni;
Kuganda kwa damu
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
9 Oktoba 2021, 12:28:13
Rejea za mada hii