top of page

Mwandishi:

Dkt. Charles W, MD

Mhariri:

Dkt. Sospeter B, MD

20 Novemba 2021, 18:35:00

Majira kwa mwenye ugonjwa wa ini

Je, unaweza tumia majira yenye vichocheo viwili ukiwa na ugonjwa wa ini?

Hapana!

Majira yenye vichocheo viwili haipaswi kutumika kwa wagonjwa wa ini au wenye dalili za ugonjwa wa ini kama vile;


  • Ugonjwa wa sirosisi ya ini

  • Ugonjwa wa ini

  • Uvimbe wa ini

  • Mwenye manjano isiyo kawaida

  • Mwenye historia ya manjano wakati anatumia majira yenye vichocheo viwili

  • Hepatitisi kali


Unapaswa kutumia njia gani kama una ugonjwa wa ini?


Kama una ugonjwa wa ini au dalili zinazoashiria ugonjwa wa ini na unataka kutumia njia za uzazi wa mpango, wasiliana na daktari wako kuchagua njia nyingine salama kutokana na hali yako.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

20 Novemba 2021, 18:35:00

Rejea za mada hii

bottom of page