top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter B, MD

Mhariri:

Dkt. Mangwella S, MD

20 Novemba 2021 20:49:00

Majira kwa mwenye VVU

Je, unaweza kutumia majira kama una VVU?

Wanawake ambao wameambukizwa VVU, wenye UKIMWI, au wanaotumia dawa za kupunguza makali ya UKIMWI wanaweza kutumia kwa usalama majira yenye vichocheo viwili.


Unashauriwa kutumia kondomu pamoja na majira yenye vichocheo viwili ili kuongeza ufanisi. Hata hivyo ukitumia kwa kwa usahihi na wakati huzuia kupata mimba.


Kondomu husaidia kuzuia maambukizo mapya ya VVU na magonjwa ya zinaa au kusambaza maambukizi hayo kwa wengine.


Kondomu pia zinatoa kinga ya ziada dhidi ya mimba kwa wanawake wanaotumia dawa za kupunguza makali ya UKIMWI (ARV).


Je, ARV inapunguza uwezo wa majira ya vichocheo viwili?


Haijafahamika katika tafiti kama iwapo ARV zinapunguza ufanyaji kazi wa majira yenye vichocheo viwili.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

20 Novemba 2021 20:53:30

Rejea za mada hii

  1. Janine Barden-O’Fallon, et al. Counseling on injectable contraception and HIV risk: Evaluation of a pilot intervention in Tanzania.

  2. Polis CB, et al. An updated systematic review of epidemiological evidence on hormonal contraceptive methods and HIV acquisition in women. AIDS. 2016;30(17). pmid:27500670

  3. Evidence for Contraceptive Options and HIV Outcomes (ECHO) Trial Consortium. HIV incidence among women using intramuscular depot medroxyprogesterone acetate, a copper intrauterine device, or a levonorgestrel implant for contraception: a randomized, multicenter, open-label trial. The Lancet. 2019. pmid:31204114.

  4. Dr Helen, et al. Contraception choice for HIV positive women. hmitchellgum.ucl.ac.uk. Imechukuliwa  20.11.2021

bottom of page