Mwandishi:
Dkt. Sospeter B, MD
Mhariri:
Dkt. Peter A, MD
20 Novemba 2021 18:59:24
Je, unaweza kutumia vidonge vya majira yenye vichocheo viwili kama una ugonjwa wa kibofu cha nyongo?
Hapana!
Wanawake wenye ugonjwa wakibofu cha nyongo au wanaotumia dawa za kutibu ugonjwa wa kibofu cha nyongo hawapaswi kutumia vidonge vya majira yenye vichocheo viwili.
Njia gani unaweza kutumia?
Unaweza kutumia njia nyingine lakini si kipandikizi au pete yenye vichocheo vya uzazi wa mpango.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
20 Novemba 2021 18:59:24
Rejea za mada hii
Etminan, et al. “Oral contraceptives and the risk of gallbladder disease: a comparative safety study.” CMAJ : Canadian Medical Association journal = journal de l'Association medicale canadienne vol. 183,8 (2011): 899-904. doi:10.1503/cmaj.110161.
AJPH. Oral contraceptives and the risk of gallbladder disease. https://ajph.aphapublications.org/doi/pdf/10.2105/AJPH.83.8.1113. Imechukuliwa 20.11.2021