top of page

Mwandishi:

Dkt. Mangwella S, MD

Mhariri:

Dkt. peter A, MD

21 Novemba 2021 15:56:10

Majira ya awamu tatu

Je, kuna tofauti gani kati ya vidonge vya awamu moja, mbili na tatu?

Vidonge vya awamu moja huwa na kiwango kinacholingana cha kichocheo estrogen na projestini katika kila kidonge.


Vidonge vya awamu mbili na tatu huwa na viwango vinavyobadilika vya vichocheo estrojeni na projestini katika vipindi mbalimbali vya duru ya kumeza majira.


Kwa vidonge vya awamu mbili, vidonge 10 vya kwanza vina dozi inayolingana, na kisha vidonge 11 vinavyofuata vina kiwango kingine cha estrojeni na projestini.


Kwa vidonge vya awamu tatu, vidonge 7 vya kwanza au zaidi vina dozi ya aina moja, vidonge 7 vinavyofuata vina dozi nyingine, na vidonge 7 vya mwisho vyenye vichocheo vina dozi nyingine.


Hitimisho

Vidonge vyote vya majira vyenye awamu yoyote ile vinazuia mimba kwa njia inayofanana. Tofauti ya athari, ufanisi, huwa ni ndogo.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

21 Novemba 2021 15:56:10

Rejea za mada hii

  1. Van Vliet, H A A M et al. “Biphasic versus monophasic oral contraceptives for contraception.” The Cochrane database of systematic reviews vol. 2006,3 CD002032. 19 Jul. 2006, doi:10.1002/14651858.CD002032.pub2. [PubMed]

  2. Percival‐Smith RK, Yuzpe AA, Desrosiers JA, Rioux JE, Guilbert E. Cycle control on low‐dose oral contraceptives: a comparative trial. Contraception 1990;42:253‐62. [PubMed] [Google Scholar]

  3. Balogh A. Clinical and endocrine effects of long‐term hormonal contraception. Acta Medica Hungarica 1986;43:97‐102. [PubMed] [Google Scholar]

  4. Briggs M, Briggs M. A randomized study of metabolic effects of four oral contraceptive preparations containing levonorgestrel plus ethinylestradiol in different regimens. The development of a new triphasic oral contraceptive. Proceedings of a Special Symposium held at the 10th World Congress on Fertility and Sterility; 1980 July; Madrid. Lancaster (England): MTP Press, 1980:79‐88.

bottom of page