top of page

Mwandishi:

WAMJW

Mhariri:

Dkt. Benjamin L, MD

10 Oktoba 2021 15:48:40

Ni watu gani hawapashwi kupata chanjo ya Korona?

Ni watu gani hawapashwi kupata chanjo ya Korona?

Chanjo zote zilizoidhinishwa na Shirika la Afya Duniani na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) zimefanyiwa tafiti kwa watu wazima na wale wenye magonjwa ya muda mrefu na zimeonekana kuwa salama, isipokuwa kuna makundi machache ambayo inashauriwa kutochanja kwa sasa mpaka Daktari akiona faida za kuchanja ni kubwa kuliko kutochanja; Mfano


  • Watu wenye historia ya mzio mkali baada ya kuchanja chanjo yoyote au kwenye moja ya kiambata cha kwenye chanjo.

  • Watoto chini ya umri wa mia- ka 18


Wajawazito

Wajawazito hawakushirikishwa kwenye majaribio ya dawa. Taarifa kamili za usalama wao bado zinafanyiwa tafiti. Ingawa wajawazito wameonekana kuwa katika hatari kubwa zaidi ya kupata ugonjwa mkali wa COVID-19 na kupelekea hatari ya kujifungua kabla ya muda na hivyo kuhitaji kinga zaidi. Hivyo inashauriwa pale ambapo itaonekana mama yupo kwenye kundi la hatari kupata COVID-19 kama vile mtumishi wa Afya wa mbele basi anaweza kupatiwa chanjo.


Mama anayenyonyesha

Hakuna tatizo kwa mama anayenyonyesha kupata chanjo na anashauriwa kuendelea kunyonyesha kwani mpaka sasa hakuna madhara yaliyoonekana kwa watoto wanaonyonya maziwa ya mama aliyechoma chanjo ya corona.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

10 Oktoba 2021 15:52:08

Rejea za mada hii

bottom of page